Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

LHRC: Theluthi mbili Zanzibar utata

$
0
0

Helen-Kijo-Bisimba

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba.

Na Mwandishi wetu

MKURUGENZI wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba, amesema watafanya uchunguzi kubaini mazingira yaliyowezesha kupatikana kwa theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Zanzibar.

Alisema ingawa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa imepitishwa, theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar haijulikani inatokana na kura gani, kwani toka awali hesabu zilionyesha kura za wajumbe kutoka visiwani zisingefikisha idadi inayotakiwa.

“Pamoja na kupitishwa hiyo rasimu, bado kuna utata wamepataje theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar, tutafuatilia tujue imetokea wapi, kwa hesabu tulizokuwa tunapiga kulikuwa hakuna uwezekano,” alisema Dk. Bisimba.

Aidha alisema hata hivyo bado wananchi wana nafasi ya kuchuja katika kura ya maoni kuangalia ni mambo yapi waliyatolea maoni waliyotoa yapo katika Rasimu ya Katiba hiyo inayopendekezwa na yapi yametolewa, na ndipo wafanye uamuzi.

“Wananchi waelewe kuwa kupitishwa kwa rasimu ya tatu si mwisho wa mchakato, bali tunawasubiri katika kura ya maoni,” alisema.

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles