Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mtuhumiwa wa mfululizo wa matukio ya ubakaji Afrika Kusini akutwa amekufa ndani ya sero.

$
0
0

south_africa_serial_rapist

 Mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa mmoja wa wawabakaji wabaya zaidi nchini Afrika Kusini Sifiso Makhubo (pichani) amekutwa amekufa katika sero ya gereza alilokuwamo.

Sifiso Makhubo ambaye alikuwa anakabiliwa na mashitaka 122 likiwemo la mauaji, mwili wake umekutwa saa chache kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi yake.

Pia alikuwa anashitakuwa kwa jaribio la kuua, kwa madai kuwa alikuwa akifahamu fika kuwa aliwaambukiza virusi vya ukimwi wale aliowabaka.

Afrika Kusini ina moja ya viwango vikubwa duniani vya matukio ya ubakaji, ambapo kwa mwaka uliopita kesi 64,000 ziliripoti polisi.

Pia ni nchi yenye idadi kubwa ya watu walioathirika kwa virusi vya ukimwi, ambapo watu milioni 5.5 sawa na asilimi 17 ya waathirika hao, wana umri kati ya miaka 15 hadi 49.

Mamlaka imesema Makhubo alikuwa mwenyewe katika sero hiyo na inaaminika alijinyonga kwa kutumia blanketi, hata hivyo wanachunguza mazingira ya kifo chake.

Alikuwa akishitakiwa kwa kuwabaka watoto 35 na wanawake wawili, kati ya Januari 2006 na Februari 2011, huku mhanga mdogo kabisa akiwa na umri wa miaka 10.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles