Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia alikuwa ni mjumbe wa Buge Maalum la Katiba, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
Aliyekuwa Makamu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza bunge hilo mjini Dodoma wakati wa ufungaji wa bunge hilo leo 2 Septemba, 2014.
Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akitoa akitoa neno la shukurani kwa wajumbe wa Bunge la Katiba na uongozi wao pamoja na uongozi wa nchi kabla ya bunge hilo kuvunjwa rasmi leo mjini Dodoma.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiwashukuru wajumbe na Watanzania kabla ya kuvunja bunge hilo rsmi leo 2 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakitoa maneno ya shukurani kwa wajumbe na Watanzania kabla ya kuvunja bunge hilo rsmi leo 2 Septemba, 2014 mjini Dodoma.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DODOMA).