Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

CUF yapongeza kura za hapana

$
0
0

magdalena-sakaya

Naibu Katibu Mkuu wa  Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara Magdalena Sakaya.

Na Mwandishi wetu

CHAMA   Cha Wananchi (CUF), kimewapongeza  Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kupiga kura ya wazi ya hapana kuhusu Rasimu inayopendekezwa licha ya kuchukua posho zote za Bunge hilo wakati wakijua fika kuwa hakuna Katiba isiyokuwa na maridhiano.

Akizungumza katika Mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Isakamuleme na Silambo vilivyopo katika Kata ya Nsungwa Wilaya Kaliua Mkoani Tabora Naibu Katibu Mkuu wa  Chama hicho Tanzania Bara Magdalena Sakaya alisema Chama hicho kinawapongeza wajumbe wote waliokataa kupiga kura ya ndio ili kupata akidi ya theluthi mbili kutoka Zanzibar licha ya kupokea posho zote huku wakijua fika kuwa hakuna Katiba isiyokuwa na maridhiano.

Alisema Chama cha Mapinduzi (CCM), kinalazimisha ili kukidhi matakwa yao kwa kutengeneza Katiba waitakayo wao bila kuzingatia maoni  ya wananchi ambayo yalikusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa muda wa mwaka mmoja na miezi nane  lakini wao wanachakachua.

“Ni aibu kubwa kwa Viongozi wote CCM waliokuwa wakijidai kuwa watapata theluthi mbili kutoka Zanzibar licha ya Vyama vya upinzani kupiga kelele kubwa kuwa hakuna theluthi mbili itakayopatikana kutoka Zanzibar na mimi niwapongeze wajumbe wote kutoka CCM waliopiga kura ya hapana jambo lililothihirisha kuwa walichokisema ni cha kweli na kimetimia”alisema Sakaya.

Alisema licha ya sh.bilioni 40 walizolipwa Wajumbe wa Bunge hilo Maalum la Katiba zingetosha kujenga  vituo vya afya na upatikanaji wa maji safi katika maeneo ya vijijini ambapo kila kukicha wakinamama wajawazito wanakufa kutokana na umbali wa kufika hospitalini.

Akijibu kero za wananchi wa Vijiji hivyo ambavyo walitaka ufafanuzi kama kweli kadi ya mama mjamzito inauzwa kwa sh.2000 na 3000 wakati limeandikwa haliuzwi Sakaya, alisema jambo hilo atalifikisha bungeni ili kupata majibu yake lakini anachokijua yeye ni kwamba huduma hiyo ni ya bure.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho Abdul Kambaya, alisema wakulima wa zao la Tumbaku wananyonywa  kutokana na kuwa na mfumo mbaya unaoongozwa na CCM ambapo haujali maisha ya watanzania walio na hali ya chini na kujenga matabaka ya walionacho na wasionacho

“Baada ya CUF kuchukua Serikali kule Zanzibar bei ya zao la Karafuu imepanda kutoka sh.1500 kwa kilo hadi sh.15000 kwa kilo kwa muda mchache tu lakini ndani ya miaka 50 ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imeshindwa kuongeza thamani ya zao hilo na kuwanufaisha wakulima ambao wanaweza kuwasomesha watoto wao kwa kutumia zao hilo “alisema Kambaya

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Tabora Kapasha Kapasha, alisema maisha wanayowaishi  wananchi hao si kwa ajili ya mapenzi ya mungu bali CCM ndio waliosababisha hayo kwani nchi hii ni tajiri lakini wanaonufaika na rasilimali hizo ni watu wachache.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles