Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Urambo kuandamana kumpinga Sitta

$
0
0

Samuel-Sitta

Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Samuel Sitta.

Na Mwandishi wetu

WAKAZI wa Urambo Mashariki wanatarajia kufanya maandamano yasiyokuwa na kikomo kupinga Rais Jakaya Kikwete asije kuingizwa kwenye mtego wa kupokea Rasimu iliyobeba maoni ya watu wenye uroho wa madaraka kama Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Samuel Sitta.

Akisoma Tamko lao kuhusu maandamano yao hayo ya kupinga vitendo vya Mwenyekiti wa Bunge hilo maalumu mbele ya  wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji  wa Wakazi hao, Isack Gerald, alisema kundi hilo la watu 12 lililosafiri kutoka Urambo hadi jijini, linawakilisha wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wazee, vijana na wanawake.

Alisema wamefikia hatu hiyo kutokana Mwenyekiti wa Bunge hilo, Sitta aikishirikiana na wajumbe wake kuondoa baadhi ya vipengele kama vile wananchi kumwajibisha Mbunge asipotekeleza majukumu yake ya kibunge kwa maslahi binafsi.

“Tunajua Sitta amesimamia uchakachuaji huu kwasababu ntu wa kwanza anayekusudia kunufaika na uchakachuaji huu ni yeye ndugu Sitta.

“Ndugu Sitta anafahamu kwa kipindi cha miaka minne ya ubunge wake hadi sasa, amehudhuria vikao viwili vya Halmashauri tangu achaguliwe na amefanya mkutano mmoja tu wa hadhara, hali inayowafanya wakose mtu wa kuyasemea na kuyasimamia madai yao ya msingi,”alisema Gerald. 

Gerald, alisema wanamtaka rais asisaini Katiba hiyo inayopendekezwa kwa sababu Bunge hilo maalum chini ya Mwenyekiti wake Sitta halikuangalia maslahi mapana ya Taifa na kizazi kijacho  na kwamba walitakiwa kuacha hadaa na kusitisha upigaji kura ya kulazimisha kupitisha rasimu isiyo ya watanzania.

Aidha, maandamano hayo wanatarajia kushirikiana na wadau wengine wenye mapenzi mema na taifa kama vile asasi za kiraia, vijana wasomi na wasiokuwa wasomi, vyama makini vilivyoonesha dhamira ya kweli ya kupinga maamuzi yaliyofanywa na Bunge hilo maalum hususan Chadema, NCCR-Mageuzi na CUF.

“Wanapinga Rais wetu mpendwa kushinikizwa kwenye mtego wa kupokea Rasimu hiyo iliyobeba maoni ya waroho wa madaraka, wenye lengo la kuichafua rekodi yake aliyokusudia kuijenga,”alisema Gerald.

Kwa upande mwingine, Gerald, alisema kudhihirisha kuwa hawna imani Sitta, kutokana na vitendo vyake uchakachuaji na kushindwa kuwahudumia wapiga kura wake, watawashauri wananchi wa Urambo Mashariki kupitia mikutano ya hadhara kutompa ushirikiano wowote wa kikazi kwa kipindi chake kilichobaki, kabla ya kumkataa rasmi katika kura za maoni ndani ya chama na uchaguzi.

Aliongeza kwa kusema wanayomba majimbo mengine kuungana nao kwa kuwanyima wabunge wo walioshiriki kupitisha Katiba hiyo ya waroho wa madaraka kwa kuhakikisha kuwa wanatumia haki yao ya kisiasa kuwawajibisha katika sanduku la kura mwaka 2015.

Vilevile kutokana na Mwenyekiti wa Bunge  hilo alivyowadhihaki na kuwadhalilisha viongozi wa kiroho,kwa hadaa ya kuwarubuni baadhi ya wajumbe wajifanye wasemaji wa  taasisi za dini  na kutoa tamko lake,na alivyowadhalilisha wandishi wa habari pamoja na kuteketeza mabilioni ya fedha za walipa kodi masikini wanamshauri asisubiri za kisheria na kisiasa zitakazoweza kuchukuliwa dhidi yake siku zijazo ni vema akajipimia na aone kama natosha kuendelea kuwa Mbunge wa Urambo Mashariki tena.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles