Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mtu mmoja nchini China amewaua watu 5 kwa kuwachoma kisu na kujeruhi wengine watatu katika jimbo la Henan.

$
0
0

knife3n-1-web

Polisi nchini China inamsaka mtu mmoja aliyeripotiwa kuwaua watu watano kwa kuwachoma kwa kisu na kujeruhi wengine watatu.

Shirika la habari nchini humo –Xinhua limesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 38 amewaua watu watatu katika kijiji na wengine wawili karibu na mji wa jimbo la Henan.

Sababu za mtu huyo kufanya mauaji hayo bado hazijajulikana.

Tukio hilo la uchomaji visu ni la hivi karibuni kutokea katika mfululizo wa mashambulio yaliyoripotiwa nchuni China.

Mtu huyo aliyetambuliwa na polisi kuwa ni Ding Jinhua, anafanyakazi katika duka la samani za mbao katika mji wa Luohe.

Baada ya kuwachoma watu hao katika kijiji, alirejea mjini dukani anakofanyia kazi na kumuua mfanyabiashara mwanamke na derive teksi.

Xinhua limesema baada ya hapo alimjeruhi dereva teksi mwingine kabla ya kuchukua teksi yake na kutokomea.

Maafisa katika jimbo hilo wametangaza zawadi kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtu huyo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles