Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mwambungu akipongeza chuo cha Mt. Joseph

$
0
0

Said Mwambungu 2

 Na Mwandishi wetu

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu (pichani), amekipongeza chuo kikuu cha sayansi ya kompyuta cha Mtakatifu Joseph Tawi la Songea kwa jitihada zake za kuendelea kupanua wigo wa kutoa huduma na kukuza elimu ya juu hapa nchini.

Mwambungu, alitoa pongezi hizo wakati wa mahafali ya tano ya chuo hicho mjini Songea, yaliyohusisha wahitimu 119 wa shahada na stashahada.

Alisema kuanzishwa kwa chuo hicho, kumesaidia kulipunguzia taifa tatizo la ukosefu wa wataalamu wa sayansi hususani katika ukanda wa kusini na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa kuanzishwa kwa chuo kikuu cha sayansi ya kilimo na teknolojia katika sekta ya kilimo ni jambo jema kwa ustawi wa nchi huku akiwataka wahitimu hao kuitumia elimu waliyoipata kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla kwa kufanya kazi kwa bidii na ufanisi.

Alisema kuwa katika maisha ya hivi sasa, hakuna njia fupi ya kufikia mafanikio katika maisha zaidi ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kudai kwamba, changamoto zilizopo katika chuo hicho zigeuzwe kuwa fursa pekee ya kujipanua na kutoa elimu bora  huku akiwataka kuboresha mawasiliano ili kukuza wigo wa utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Aidha, amewaomba wanafunzi wa chuo hicho, kuombea amani hususani katika kipindi hiki kigumu ambacho taifa linaingia kwenye mchakato wa uundwaji wa katiba mpya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya chuo hicho, Askofu John Ndimbo, alisema kuwa anajisikia fahari kuona chuo hicho kinazalisha wataalamu wengi wa sayansi ukanda wa kusini huku akidai kuwa elimu ni tunu kubwa ya maendeleo.

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Latest Images

Trending Articles



Latest Images