Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mitambo ya kuzalisha umeme katika bwawa la Kidatu, mkoani Morogoro mwaka 2011.Kushoto ni meneja wa TANESCO wa mkoa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera.
Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), limesema Mgodi wa wa kufua umeme, uliojengwa Kidatu, Morogoro 1975, bado zinauwezo wa kuzalisha nishati hiyo kwa kiwango cha kutosha.
Kauli hiyo ilitolewa, Meneja wa Mgodi huo Injinia Joseph Lyaruu, wakati ziara ya wandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa lengo la kujionea kazi zinavyofanyika katika mgodi huo.
Alisema, uwezo huo ulitokana na jitihada za Tanesco kuendelea kuboresha mgodi huo kwa kufunga mashine nne ambazo zinauwezo wa kuzalisha umema kwa ufanisi ambao unakwenda sambamba na ongezeko la wateja kila mwaka.
“Sio kweli kama mtambo hauwezi kuzalisha umeme kama inavyodhaniwa, na baadhi ya watu bado unao uwezo wa kufanyakazi katika kipindi cha miaka 50, hata nchini India iko mitamboambayo imefanyakazi zaidi ya miaka 50,”alisema Injinia Lyaruu.
Lyaruu, alisema Watanzania hawana haja yakuwa na wasiwasi kuhusu uzalishaji katika mgodi huo, kwasababu shirika kwa kushirikiana na wahisani wamo katika mkakati kubadili baadhi ya vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwepo tangu unajengwa.
Akizungumzia kuhusu hali ya maji, Lyaruu, alisema Watanzania watarajie kupata huduma hiyo kwa ufanisi na bila kikomo kwa sababu kipindi hiki maji ya kutosha yapo.
“Hapa kazi hazisimami kama mnavyoona muda wote tunafanyakazi ili huduma hii isikosekane na hii inatokana na Tanesco kutambua umuhimu wa huduma hii katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini,”alisema Injinia Lyaruu.
Alizitaja baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili katika uzalishaji wa huduma hiyo, kuwa ni uhaba wa maji, shughuli za kibinadamu karibu na mito inaingia kwenye mabwawa na uchepushaji wa maji kwa ajili ya kilimo na nyingine.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu, Rashid Msingwa, alisema katika mgodi huo kunawafanyakazi 104, ambao wanafanya kazi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za jamii.