Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

JK awasili Marekani kuhudhuria mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York. Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.

us1

Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali

us2

Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali.

us3

Rais Kikwete akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakati alipokuwa anaondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuelekea Marekani Septemba 15, 2014. 

us4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili New York, Marekani. Kulia Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifuatiwa na Mama  Upendo Manongi Septemba 16, 2014.

us5

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.

us6

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Tanzania  baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.  (PICHA NA IKULU).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles