Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

TANESCO yawatesa wananchi wa Mwanagati Kitunda kwa kukosekana umeme siku tatu mfululizo

$
0
0

tanesco

Na Mwandishi wetu

Kwa habari tulizozipokea hivi punde toka kwa wananchi wa Mwanagati-Kitunda jijini Dar es Salaam zinasemekana kwamba wananchi wa maeneo haya hawana umeme kwa siku 3 mfululizo usiku na mchana mpaka sasa na hakuna taarifa zozote toka shirika la umeme Tanesco kuelezea hali hii inayoendelea mpaka sasa.

Wananchi mbalimbali wakielezea, walisema hawakupata taarifa yoyote ile toka Tanesco na mpaka sasa wengi wao wamepata hasara kubwa kibiashara kutokana na tatizo ili na upande mwingine akina mama wengi tuliowahoji wamesema wengi wao wana watoto wachanga hivyo imekuwa wakipata shida kubwa kama wazazi kwa joto kali kutokana na kukosekana kwa umeme na pia kwa kuongezeka kwa vibaka nyakati za usiku.

Mbali na matatizo hayo, Mji huu mpya ambao una chanzo chao cha kipekee kikubwa cha maji ambapo kinategemea umeme katika uzalishaji wa maji na kufanya wananchi hawa kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi.

Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la umeme Tanesco ili kuelezea tatizo ili kwa wananchi wa Mwanagati – Kitunda zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Latest Images

Trending Articles



Latest Images