Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu ulioanza jana katika ukumbi wa Karimjee na kufunguliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete kesho.
Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole, wabunge wa EALA kutoka Tanzania Twaha Taslima na Shy Rose Bhanji.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Tanzania, Adam Kimbisa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dar es Salaam jana, juu ya mkutano wa kwanza wa Bunge la tatu unaofanyika ukumbi wa Karimjee. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Dk. Margaret Nantongo Zziwa,wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Twaha Taslima na Shy Rose Bhanji. PICHA ZAIDI–FATHER KIDEVU BLOG