Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Serikali yakiri sheria ya ndoa ya 1971 haifai

$
0
0

DSC_0104

Mgeni Rasmi katika utambulisho wa kampeni ya kitaifa kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe,  akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa kufanyia marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka 1971.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

.Wadau watambulisha kampeni ya kupambana tatizo la ndoa za utotoni

Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania

SERIKALI ya Tanzania imekiri kwamba Sheria ya Ndoa ya 1971 ni kikwazo katika kupambana na tatizo la ndoa za utotoni na inajipanga kuifanyia marekebisho ili kulinda haki na sera ya mtoto wa Tanzania iliyopitishwa na Bunge mwaka 2009.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa kutambulisha kampeni mpya ya kitaifa ya kupinga ndoa za utotoni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe, amesema kwamba serikali inaridhia kuendesha kampeni ya kupambana na kuzuia ndoa za utotoni nchini.

“Utafiti unaonyesha kwamba kati ya wasichana watano wawili kati yao kupata mimba kabla ya kufikia umri wa miaka 18 kila mwaka nchini Tanzania,” amesema Bi Maembe

Amesema kwamba serikali kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo watatizama vyanzo vya ndoa za utotoni kuanzia kwenye masuala ya kiuchumi, kijamii, mila na desturi na sababu zingine zinazochangia ukuaji wa tatizo.

“Ndugu zangu tatizo la ndoa za utotoni si swala la kuachia serikali peke yake ni kwa kushirikiana na jamii nzima tunaweza kupambana na kuondoa tatizo la ndoa za utotoni kwa wasichana wa Tanzania,”

DSC_0057

Mwakilishi kutoka, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utambulisho wa kampeni ya kitaifa ya kupinga ndoa za utotoni nchini (National Ending Child Marriage Campaign). Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole na Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN-Women) nchini, Anna Falk-Collins akifuatiwa na Mgeni Rasmi katika utambulisho wa kampeni ya kitaifa kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe.

“Na ukitizama kwa undani wasichana wengi wanapoteza maisha wakati wa kujifungua ni wenye umri chini ya miaka 18 na wengi wao wanapata magonjwa ya fistula na ni kundi hatarishi la kupata maradhi ya magonjwa ya zinaa na ukimwi,” aliongeza

Bi Maembe aliongeza kwamba serikali inaangalia uwezekano wa kupitia sheria, sera na mila na desturi katika kuhamasisha jamii juu ya uelewa wa tatizo la ndoa za utotoni na madhara yake katika ustawi wa jamii na watu wake.

Alifafanua kwamba ni muhimu kwa jamii kuanza kubadilika juu ya mila na desturi zinazochochea ndoa za utotoni nchini ili watoto wa kike wapate nafasi ya kwenda kusoma hadi vyuo vikuu.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dkt, Natalia Kanem amesema kwamba Tanzania ndio ina idadi kubwa ya ndoa za utotoni kwa wasichana kabla ya umri wa miaka 18.

Alifafanua kwamba nchini Tanzania mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni ni mkoa wa Mara, Shinyanga, Dodoma, Lindi na Tabora kwa hiyo ni muhimu kwa jamii kuanza mapambano ya dhati dhidi ya mimba za utotoni nchini Tanzania.

“kuna mambo mengi yanachangia kwa kiasi kikubwa tatizo la ndoa za utotoni ikiwemo sheria, mila na desturi na sababu zingine za kiimani,” aliongeza.

DSC_0016

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka (kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zitakazoendeshwa Mkoani Mara. 

Amesema kwamba kupitia kampeni hiyo mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Wizara ya wanawake, Taasisi ya Mamna Graca Machel, na Jukwaa la Utu wa Watoto wataanzisha klabu za mashuleni ili kutoa mafunzo na madhara ya ndoa za utotoni kwa wasichana nchini nzima.

Dkt. Kanem amesema kwamba kupitia kampeni hiyo wasichana watafundishwa mambo ya afya ya uzazi, magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI na madhara ya mimba za utotoni kiafya na kisaikolojia.

Aliongeza kwamba tatizo la ndoa za utotoni ni tatizo la dunia nzima kwa mantiki Umoja wa Mataifa kupitia malengo yake ya millennia iliamua kuweka jambo la jinsia, afya ya mtoto kama vigezo vya kuondokana na umaskini katika nchini zinazoendelea.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TAMWA, Bi Valenrie Msoka amesema kwamba kampeni hii ni ya kipekee nchini na ni muhimu kwa wadau wote wa maendeleo kuunga mkono ili kutokomeza kabisa tatizo la ndoa za utotoni nchini.

Amesema kwamba kampeni hii itawashirikisha Jeshi la Polisi, Wizara, Viongozi, Madhehebu ya dini na majaji katika juhudi za kufikisha ujumbe kwenye ngazi za maamuzi nchini Tanzania.

“Ni imani yangu kwamba wadau wakubwa katika mapamban dhidi ya ndoa za utotoni ni waandishi wa habari ambao wana kila sababu ya kuandika na kuelimisha jamii umuhimu wa mtoto wa kike kupata elimu,” amesema Bi Msoka.

DSC_0207

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akitoa nasaha wakati wa utambulisho wa kampeni hiyo.

DSC_0176

Mwakilishi wa Taasisi ya Graca Machel, Bernard Orimbo akitoa mifano ya taarifa mbalimbali kutoka nchi za kusini mwa jangwa la sahara zilivyoathirika na tatizo la ndoa za utotoni na bara la Afrika kiujumla na madhara ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

DSC_0045

Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Watoto, Koshuma Mtengeti akizungumza na waandishi wa habari ni kwa njinsi gani sheria na tamaduni zinavyochochea ndoa za utotoni nchini na umuhimu wa kuendesha kampeni ili kujenga uelewa kwenye jamii madhara ya ndoa za utotoni kwa watoto wa kike na taifa kwa ujumla.

DSC_0261

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.

DSC_0273

Mwandishi wa habari kutoka EATV, Noah Laltaika akiuliza swali kuhusiana na wilaya Ngorongoro ya jamii ya kifugaji ya wamasai iliyokithiri kwa ndoa za utotoni ambapo ameiomba Serikali pia iweze kuifikia jamii na kutoa ya elimu ya kutosha kupitia kampeni hiyo.

DSC_0075

Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wengine wa habari  na wadau kutoka taasisi na mashirika mbalimbali ya haki za watoto wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zilizofanyika jijini Dar es Salaam kampeni hizo zitaendeshwa Mkoani Mara.

DSC_0234

Mwandishi wa habari wa ITV, Jackline Silemu akiuliza swali kwa mgeni rasmi (hayupo pichni) wakati wa utambulisho wa kampeni hiyo.

DSC_0180

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka (kulia) akifurahi jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole.

DSC_0214

Mmoja wa wadau akipitia kijiradi kinachoelezea athari za ndoa za utotoni kwa watoto.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles