Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akifungua semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) leo jijini Dar es salaam.
Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba, amewataka wafanyabiasha nchini, kutengeneza miradi ambayo inatambulika ili iwe rahisi kukopeshwa fedha.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kufungua semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo Mashariki na kusini mwa Afrika (TPA).
Mwigulu alisema kuwa, kumekuwapo na changamoto nyingi za wafanyabiasha kutokukopeshwa na mabenki kutokana sababu zinazoonesha kuwa wazi fedha hazitarudishwa.
“Nawataka wafanya biashara wote, kutumia fursa hii kujifunza mbinu na kutengeneza miradi ambayo itaweza kukopesheka kiurahisi” alisema.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) Admassu Tadesse akitoa maelezo ya jumla juu ya utendaji kazi benki ya hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa semina ya wafanyabiashara na benki hiyo.
Aliongezea kuwa, PTA ni benki ya Kiafrika na inafanyakazi nzuri kwa nchi zote iliyopo, ambapo inaonesha inakua kwa zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka kwa miaka kadhaa hadi sasa na imekuwa na mizania ya Dola za Kimarekani mil. 2.8 ikiwa miongoni mwa benki za maendeleo zinazofanya vizuri katika bara la Afrika.
“Katika tano bora katika nchi za afrika, nchi yetu ni miongoni mwa nchi tano zinazonufaika na benki hii pamoja na Nambia, Zambia, Malawi na sudani” alisema.
Kwa upande wake Rais na Mtendaji Mkuu wa benki ya PTA Admassu Tadesse amesema kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele na ni mwanachama hai ambapo imekuwa mfano mzuri kwa nchi wanachama kwa kutoa michango mbalimbali kwa wakati.
Zaidi ya hayo, Tadesse amesema kuwa benki hiyo mwaka huu inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu ili washerehekee na Watanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akifunga semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) leo jijini Dar es salaam ambapo amesistiza kuwa Wafanyabishara nchini watumie fursa ya semina hiyo ili waweze kuandaa mikakati ya kibiashara ya muda mrefu, wa kati na muda mfupi waweze kujiletea maendeleo yao na nchi kwa ujumla.
Mkurugenzi wa DoubleTree by Hilton Hotel, Ayaz Ali Jivraj akiuliza swali juu ya namna wafanyabiashara wanavyoweza kunufaika na huduma za kibenki kupitia Benki ya PTA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na benki hiyo leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Maafisa wa Serikali na wafanyabiashara wakiwa kwenye semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ufungzi wa semina ya wafanyabiashara leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na kulia ni Rais na Mtendaji Mkuu wa benki ya Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) Admassu Tadesse.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya ufunguzi wa semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA).
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (kulia) akibadilishana mawazo na Rais na Mtendaji Mkuu wa benki ya Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) Admassu Tadesse (katikati) mara baada ya ufunguzi wa semina ya wafanyabiashara leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile.(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO).