Na Mwandishi wetu
Wanawake nchini wametakiwa kutokuwa na woga katika kusimamia mambo mbalimbali ya maendeleo.
Wametakiwa kuwa katika mstari wa mbele hasa katika kusimamia masuala ya siasa, uchumi na ya kijamii kwa nguvu zote.
Hayo yalielezwa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Bara,Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Eva Mwingizi,wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya wenyeviti na makatibu wa UWT, wilaya ya Kinondoni.
Alisema kwa kujiweka nyuma kutasababisha hata uwiano sawa wa asilimia 50 kwa 50 kutoweza kufikiwa kutokana na wao wenyewe pia kushindwa kujitokeza kugombea nafasi mbali za uongozi.
Alisema ingawa UWT ipo kisiasa lakini walifikiria kuwainua kina mama kwa kuanzisha kitengo cha miradi, ambapo pamoja na mambo mengine kinawaunganisha na taasisi mbalimbali za mikopo ilikuinua biashara zao.
Naye muandaaji wa warsha hiyo, Diwani wa Viti Maalum Msasani, Kuruthum Sagamiko, alisema lengo ni kuwajengea uwezo wanawake hao wanaotoka katika kata, kwakuwandiowenye watu .
Licha ya kupata mafunzo ya kisiasa, Kuluthum alisema pia kunamkufunzi wa mamboya biashara, ili kuleta msukumozaidi,kwa kuamini kuwa mwanamke mwenye uchumi ananguvu zaidi.
Alisema katika wilaya hiyo ya Kinondoni tayari wamepoteza majimbo mawili na kata 11, hivyo kupitia wanawake hawa, wenye uelewa itakuwa rahisi kurudisha maeneo hayo yaliyopotelea kwa upinzani.