Mke wa mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William amejifungua mtoto wa kiume.
Kate Middleton amejifungua mtoto huyo katika hospitali ya St. Mary’s, iliyoko magharibi mwa London, akiwa na uzito wa kilo 3.79.
Jinsia ya mtoto huyo haikujulikana kipindi chote cha ujauzito, kwa sababu Kate na William hawakutaka kujua jinsia ya mtoto wao, hadi pale atakapozaliwa.
Kulingana na utamaduni wa Uingereza, taarifa rasmi za kuzaliwa kwa mtoto huyo, zilitolewa nje ya milango mikuu ya kasri la Buckingham, jana jioni.
Mtoto huyo ataitwa “Kendall Charles Cambridge”.