Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame, amefariki dunia katika hospitali ya AMI Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kuugua na kulazwa kwake, zilianza Mwezi uliopita, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete alimtembelea hospitalini.
Picha, Rais Kikwete alipofika kumjulia hali Hayati Lewis Makame, Julai 27 mwaka huu Jijini Dar.
