Miss Kanda ya Kati Dorice Mollel katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe Philip Marmo nje jengo la ubalozi wa Tanzania jijini Berlin alipotembelea ubalozi huu akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 (hawapo pichani) kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere.
Baada ya kutembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini Berlin, Mhe. Marmo aliwaelezea historia ya ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania ambapo nchi hiyo imekuwa miongoni mwa wadau wa maendeleo kwa kutoa misaada mbalimbali nchini kwetu.