Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mama Asha Bilal azindua “Omo Fast Action” jijini Dar leo

$
0
0

1

 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal akitoa hotuba yake wakati alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Unilever Tanzania Limited, leo hii imezindua rasmi toleo jipya la sabuni yake ya kufulia ya Omo ambayo inaondoa madoa sugu haraka zaidi na kuacha nguo zikinukia vizuri. Sabuni hiyo mpya ya ‘Omo Fast Action’ imezinduliwa katika hafla iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mheshimiwa Mama Asha Bilal, mke wa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wawakilishi kutoka wizara ya Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Mstahiki Meya wa Ilala, Jerry Silaa, Wawakilishi kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, Marc Engel.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Marc Engel, Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, alisema uzinduzi huu wa sabuni ya OMO Fast Action unaileta teknolojia ya kisasa kabisa nchini, kwani OMO Fast Action mpya inaondoa madoa sugu haraka zaidi, ina manukato mazuri na yanadumu kwa muda mrefu, huku ikiiacha mikono laini na haivubazi nguo.

13

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever kwa Afrika Mashariki,Marc Engel akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

“Sisi Unilever tunatambua shughuli nyingi zinazowakabili wakinamama majumbani, ‘Omo Fast Action’ ndio suluhisho lao kwani sasa ina uwezo wa kusafisha nguo na zikawa safi kabisa katika kipindi cha dakika moja tu. Sabuni hii ambayo sasa inapatikana katika paketi zenye muonekano mpya, ni laini kwa mikono yako na inaacha nguo zikiwa na manukato ya kunukia vizuri” alisema Engel.

Engel pia aliwakumbusha wakinamama wasiwakataze watoto kuchafuka wanapocheza kwani wakicheza hawakusanyi uchafu peke yake bali pia ndio wanajifunza na kugundua vitu mbalimbali vinavyowazunguka. Kama kauli mbiu ya OMO inavyosema, ‘Uchafu ni Mzuri’, kinamama wa kitanzania sasa wanaweza kuwapa watoto uhuru wa kucheza na kujifunza bila kuwa na wasiwasi wa nguo kubaki na madoa sugu baada ya kufuliwa.

Naye mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Mheshimiwa Mama Asha Bilal aliipongeza kampuni ya Unilever kwa jitihada zao katika kuboresha maisha ya kinamama na watoto siku hadi siku.

Mama Bilal pia alipongeza uboreshaji wa sabuni ya Omo kwa kuwawezesha kinamama kufua kwa muda mfupi sana na hivyo kupata nafasi kushiriki katika shughuli za maendeleo. “Katika ulimwengu wa sasa, mwanamke hakai nyumbani tu kama golikipa, mwanamke anapaswa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kusaidia kuongeza pato la familia. Mimi kama mama, naelewa kuna changamoto nyingi za majukumu ya familia, lakini nahamasisha kinamama kote nchini, tuamke, tupambane, ili kuimarisha nafasi yetu katika familia na jamii yetu kiujumla.”

20

Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Unilever Tanzania,Teresia Kamweru akitoa shukrani zake kwa Mgeni Rasmi na Wadau mbali mbai walioshiriki kwenye hafla hiyo ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

11

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Asha Bilal akipokea zawadi ya picha ya mchoro kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever kwa Afrika Mashariki,Marc Engel mara baada ya Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.  

7

Warembo wakiwa na mfano wa Sabuni ya OMO FastAction wakati wa Uzinduzi wa Sabuni ya kufulia ya OMO FastAction uliofanyika rasmi leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.(Picha na Othman Michuzi Blog).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles