Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Global Education Link kusaidia mikopo vyuo vikuu

$
0
0

IMG_7289

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Global Education Link (GEL), Abdumaliki Molle.

Na Mwandishi wetu

TAASISI ya Global Education Link (GEL), inayojishughulisha na masuala ya elimu ya juu, imesema ipo tayari kutoa mikopo kwa wazazi na walezi wanaohitaji watoto wao kwenda kusoma vyuo vikuu nje ya nchi, ili kuwezesha vijana kuingia katika soko la ajira duniani.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkurugenzi wa Udahiri wa taasisi hiyo, Zakiah Nassoro, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, wakati wa semina ya wasomi wa vyuo vikuu jijini hapa.

Alisema Taasisi yake hiyo ya Global Education Link ambayo hadi sasa imefanikiwa kusomesha watoto 4,000 kuanzia 2006 katika vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi, imejizatiti kutoa msaada huo wa kielimu ili kuwezesha vijana wengi kufikia malengo yao kwa kuingia katika soko la ajira.

“Global Education Link ambayo imeanzishwa mwaka 2006 imejiwekea utaratibu wa kutoa mikopo ya kuanzia asilimia 50 hadi 70 kwa mzazi au mlezi anayehitaji mwanaye kwenda kusoma Chuo Kikuu chochote Duniani.

“Lakini tunawaomba sana wazazi washirikiane na sisi Global Education Link kutoa elimu kwa watoto wao wanaokwenda kusoma nje ya nchi, ili wasijiingize kwenye biashara ya dawa za kulevya,” alisema Mkurugenzi huyo wa Udahili, Nassoro.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Nassoro, hadi sasa taasisi yake imeshapokea maombi 900 ya watoto wanaohitaji usaidizi wa taasisi hiyo kwenda kusoma elimu ya juu nje ya nchi, na madhumuni yao ni kutaka kufikia melengo katika soko la ajira.

Aliwaomba Watanzania kutumia taasisi hiyo kusomesha watoto wao wanaohitaji kwenda kusoma vyuo vikuu vilivyopo nje ya nchi, kwani taasisi yake hiyo imekuwa msaada mkubwa sana katika kupanua sekta ya elimu na ajira kwa vijana.

Mkurugenzi Nassoro aliongeza kwa kusema: “Global Education Link inao uwezo wa kubeba gharama za mtoto anayeshindwa kuendelea na masomo yake huko Ugaibuni, lakini kwa makubaliano maalumu na mzazi au mlezi wa mtoto husika, na si vinginevyo”.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles