Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

TASAF kunusuru kaya masikini

$
0
0

DSC04088

Na Mwandishi wetu

Mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Manyoni, Mkoani Singida, umeanndikisha kaya 8,113 kati ya kaya 8,404 zilizotambuliwa na mpango huo katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Julai,mwaka huu.

Kaimu Mratibu wa TASAF Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida, Bwana Herilabert Sagali alisema mpango huo ulianzishwa kwa malengo mawili ambayo ni pamoja na kutambua kaya maskini na kuandikisha kaya maskini.

Kwa mujibu wa mratibu huyo malengo ni kujenga uwezo pamoja na kuwezesha kaya maskini kuongeza kipato,fursa na uwezo wa k ugharamia mambo muhimu kama vile elimu na afya pamoja na kuboresha maisha kwa ujumla.

Hata hivyo Bwana Sagali aliweka wazi kuwa wilaya hiyo ililenga kupata kaya 13,995 na kwamba katika zoezi la kutambua katika vijiji 61 vilivyokuwa katika mpaango huo,walilazimika kuvigawa katika makundi matatu.

Akifafanua zaidi mratibu huyo alisema katika awamu ya kwanza walianza na vijiji 21 wakati kwa awamu ya pili vijiji 20 vilihushwa na katika awamu ya tatu vijiji 20 vilihusishwa.

Mratibu huyo wa TASAF alibaianisha pia kwamba katika zoezi la utambuzi,mpango huo ulitambua kaya 8,404 lakini baada ya zoezi la kuandikisha  walipata jumla ya kaya 8,113.

“Labda kwa ufupi  ndo hivyo na kwa sasa hivi tunasubiri kwa ajili ya fedha za ili ziweze kuwafikia walengwa…na katika kuongezea hizi fedha  zinaletwa kwa ajili ya kuwafikia wale walengwa”alifafanua.

Aidha Bwana Sagali alisema fedha hizo wanazozisubiri zinaletwa ni aina ya ruzuku na kwamba ruzuku hizo zitakuja katika malengo mawili,ambayo aliyataja kuwa ni pamoja na ruzuku yenye masharti na ruzuku isiyokuwa na masharti.

“Kwa ruzuku isiyokuwa na masharti  mtu atapata shilingi 8,500/= kwa mwezi na hivyo kwa miezi miwili atapata shilingi 17,000/= na kwa ruzuku yenye masharti kila kaya kwa wale ambao hawajaandikishwa shule ili waweze kwenda shule na kwa wale ambao hawajahudhuria kliniki ili waweze kuhudhuria ni shilingi 17,000/= kwa mwezi na kwa miezi miwili iwapo muhusika atatimiza masharti yaliyowekwa atapata 34,000/=”alisisitiza Mratibu huyo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Itigi Mjini, Bwana Ally Minja akizungumzia mpango huo katika kata yake alifafanua kuwa TASAF awamu ya tatu kupitia mpango  wake wa kuwezesha kaya maskini umetambua kaya 315 zitakazofaidi kwa kupata ruzuku ya kaya na ruzuku ya kusaidia watoto ambao watakuwa wanasoma katika shule za msingi.

Alisema kutokana na kaya hizo 315 zilizotambuliwa tayari wameshapata hati zao za utambuzi,wamekwishaingizwa kwenye mfumo na hivi sasa wanasubiri malipo ambayo wakati wowote yanaweza yakafika.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Latest Images

Trending Articles



Latest Images