Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta.
Na Mwandishi wetu
Mwinjilisti wa Kanisa la TAG liliko Mbagala wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Medad Kyabashasa, amesema kitendo cha Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta kuunda Kamati ya maridhiano ni kitendo cha kuwahadaa Watanzania.
Hadaa hiyo ni yakutaka kuwafanya wajumbe wanaopigania Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao wametoka nje ya bunge hilo kupinga ubabe unaofanywa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi, waonekane ni wakorofi.
Medadi, alisema Mwenyekiti huyo anafahamufika fika kuwa Ukawa hawataweza kuhudhuria kwenye kamati hiyo ya maridhiano kutokana na hata yeye mwenyekiti kuwa sehemu ya mgogoro huo unaondelea.
Alisema wakati bunge hilo maalumu lilipokuwa likiendelea Sitta alishindwa kuwakemea wajumbe wa CCM wakati walipokuwa wakiwaporomoshea matusi wajumbe wenza.
Mbaya zaidi Sitta alikuwa akiunga mkono matusi hayo kwa kusema”Mweshimiwa meda wako unalindwa wajumbe tutulie amalizie akimanisha matusi”.
Kutokana na hali hiyo ya sintofahamu Sitta anafanya propaganda ambayo baadae ili waje waitumie na chama chake pamoja na Rais wake kwa kuupotosha umma kuwa Ukawa umekataa maridhiano.
“Hivi tangu lini mporwaji na mporaji wa wakakaa papomoja kufikia maridhiano huu ni uchajanja wa CCM kukwepa hoja za msingi”alisema Kyabashasa.
Kyabashasa, alisema kote huko wanakopita CCM ni kutaka kuwapotezea muda Watanzania kwa sababu sababu chanzo cha mgogoro huo wanakijua.
“Maridhiano hayo ni maridhiano gani ni Ukawa wakubali ukiukwaji wa sheria, kanuni, matusi baadala ya kujadili rasimu ya katiba, katika hili hakuna haja ya kupoteza muda wa kuunda kamati ya maridhiano lazima CCM kujadili maoni ya wananchi” Kyabashasa.
Vilevile, aliwahadharisha wanasiasa hususasani wale wanaotoka CCM kuwa wasipende kuvuruga amani ya nchi kisha kumgeuza mungu kikaragosi kwa kuwaambia viongozi wa dini waombee amani.