Vinywaji vya OH 2 vikiwa kweywe friji.
Na Mwandishi wetu,
KINYWAJI chenye ladha laini ya kupunguza uchovu na kuongeza akili na nguvu mwilini cha OH2 Energy Drink ‘Great Taste’ or ‘Test you want’ kimekuwa gumzo kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya biashara ya 38, Dar es Salaam ‘Sabasaba’ yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa watu mbalimbali kukinunua kwa wingi.
Kwa mujibu wa Marketing Manager wa kinywaji hicho, Oliver alieleza kuwa, kinywaji hicho chenye ladha laini na kinapunguza uchovu kwa mtumiaji anapokinywa, kimekuwa faraja kubwa. “Bidhaa yetu ya kinywaji cha OH2 Energy drink, kinaongeza nguvu na akili kwa mtumiaji” alisema Oliver.
Mmoja wa warembo akiwa amefurahia kinywaji cha OH2 energy, akiwa kwenye pozi ndani ya Saba saba
Aliongeza kuwa, kinywaji hicho kinatoka Uswis, na hakina kilevi na ni kitamu ile mbaya huku sukari yake ikiwa ni ya wastani zaidi ya nusu ya vinywaji vingine vya Energy na ladha yake imetulia.
Hata hivyo, alisema kwa sasa kinywaji hicho kinapatikna Dar es Salaam na Zanzibar, huku kwa Dar es Salaam wakipatikana Kunduchi, Kinondoni na usambazwa na kampuni ya OH2 Beverage Ltd.
Pia alisema kinywaji hicho kinapatikana kwenye baadhi ya Bar na Klabu zote burudani hapa nchini.