Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Libe aungana na iftar ya Tanzanian Muslim Community in Washington DC Metro(TAMCO)

$
0
0

Na  Abou Sharty Washington DC

Mgombea wa Urais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, Bwana Liberatus Mwang’ombe “Libe”, siku ya Jumapili July 6, 2014 alipata fursa ya kujumuika katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Tanzanian Muslim Community (TAMTCO), iliopo Washington DC Metro,  kwa ajili ya kuonyesha umoja na mshikamano dhidi ya Jumuiya ya mbali mbali ziliopo hapa DMV.

10524472_10154309166070247_469083183_n

 Mgombea wa Urais wa Jumuiya ya waTanzania DMV, Bwana Liberatus Mwang’ombe “Libe”. (wapili kulia) akipata picha ya pamoja na  waumini wa  Tanzanian Muslim Community in  (TAMCO) Siku ya Jumapili July 6, 2014 ndani ya ukumbi wa Indian Spring ulipo Silver Spring Maryland.

Bwana Liberatus Mwang’ombe, alisema kuwa ”Alifurahishwa sana na kitendo cha ushirikianao huo wapamoja unaofanya na Jumuiya ya waIslamu, kwa ushirikiano wao na  kupata futari ya pamoja pale ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao hukusanyika familia mbalimbali na kuweza kupata chakula cha pamoja, ” nilijisikia nipo nyumbani na kuwa na furaha  na kila mmoja aliehudhuria katika futari hiyo” alisema

Katika kampeni za uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV, zinazoendelea kwa kasi mjini hapa Bwana Liberatus Mwang’ombe, mwezi uliopita, siku ya jumamosi June 28, katika kiwanja cha Meadowbrook Park, alipata fursa ya kufanya mkutano wa sera zake za kuleta maendeleo kwa wakaazi wa Jumuiya ya waTanzania DMV, pindi atakapochaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya, katika mkutano huo aliweza kushirikiana baadhi ya wagombea mbali mbali kwaajili ya kampeni za kuleta maendeleo dhidi ya waTanzania, waishio hapa DMV.

 Bwana Libe aliweza kuzungumzia kuhusu  marekebisho ya ubadilishaji wa vifungu vya katiba zinavyomkaba Mtanzania anaeishi hapa DMV, kulipa ada, ndipo apate fursa ya kupiga kura, alisema vifungu hivyo atakapochaguliwa atakuwa tayari kuviondoa, pale tu atakapokubaliana na wanajumuiya kutokana na kutowapa furasa watu waTanzania wanaoishi hapa DMV kutopiga kura hadi walipe ada na kuwa wanachama hai ndipo wapige kura wakiwa kma wazawa halisi wa Tanzania.

Mara baada ya ftari Bwana Liberatus Mwang’ombe ambae ni mgombeya wa Jumuiya ya waTanzania DMV alisema juu ya mfumo mzima wa ushirikiano wa kuendesha Jumiaya hiyo bila ya kujali idikadi ya mtu yoyote ile na kuwa kitu kimoja na kuonyesha umoja na mshikamano kwaajili ya kumjanyua mTanzania alie hapa DMV, pamoja na kuitangaza nchi yetu Tanzania na kuwa wazalendo wa ukweli na wakujitolea pale mTanzania mara tu atakapofikwa na matatizo ya aina yoyote yale, aliongea hayo na blog ya swahilivilla mara tu baada ya kungana na iftar ya Tanzanian Muslim Community in Washington DC Metro (TAMCO) na huku akisisitiza kuomba kura zenu pindi mtakapolipa aida za upigaji kura zenu, na kumchagua kiongozi mnaemtaka.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles