Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Jerry Slaa kukabidhi zawadi kwa wateja wa banda la MeTL Sabasaba

$
0
0

IMG_1291

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa.

Na Mwandishi Wetu

WATEJA wanaotembelea banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea  kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere,  barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, kesho Jumatatu  wanatarajiwa kuchezeshewa  droo maalum itakayotoa zawadi mbalimbai ikiwemo pikipiki.

Katika droo hiyo  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi  na atakabidhi zawadi kwa wateja mbalimbali watakaojishindia zawadi hizo.

 Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni  ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer  alieleza kuwa,  droo hiyo ni maalum kwa ajili ya wateja wote waliopata kutembelea  banda hilo tokea siku ya kwanza na kujiorodhesha majina yao

Fatema alisema MeTL Group imeamua kutoa zawadi  hizo kama shukrani  na kujitangaza zaidi kwa wateja na wananchi waliopata kutembelea na kununua bidhaa  za MeTL Group.

“Kwa ubora wa bidhaa zetu za MeTL Group,  kama  inavyojulikana,  ‘The People’s  Brand’,   kwa droo hii wateja wetu watafurahia  kwa zawadi hizo nono” alisema Fatema.

Katika droo hiyo, zawadi kuu ni pamoja na Pikipiki,  zawadi za khanga, vitenge, mashuka, sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kupikia, unga na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.

Aidha, MeTL Group  imetambulisha rasmi vinywaji  vyake vipya kwenye maonyesho hayo ya Saba Saba, ikiwemo kinywaji kinachopendwa na wengi kwenye maonyesho hayo, MO Cola,  MO Portello na MO Malt.  Vingine ni  MO  Lemon Mint,  MO chungwa na MO Bomba  (Energy  drink).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles