Waheshimiwa, William Lukuvi (kulia), Anna Abdallah (katikati) na Tundu Lisu wakibadilishana mawazo , Bungeni Mjini Dodoma.(Picha na Maktaba).
Na Mwandishi wetu
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, Kesho atakuwa katika banda la ofisi za Bunge ili kutoa maelezo kwa wananchi kuhusiana na namna ya utendaji wa Bunge.
Akizungumza jana katika banda la ofisi za Bunge lililopo viwanja vya maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, Ofisa Habari wa Bunge, Owen Mwandumbya, alisema kuwa Makinda atambatana na viongozi wengine wa bunge ili kuwaeleza wananchi shughuli mbali mbali za Bunge.
Aliwataja viongozi hao kuwa watakaowahudumia wananchi watakaofika katika banda hilo ni William Lukuvi Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu.
Alisema kuwa viongozi hao watawaeleza wananchi hatua za utungaji sheria, kutoa maelezo kuhusiana na siwa kwanini inaheshimika na mambo yahusuyo Bunge.
Mwandumbya alisema kuwa kwasasa ofisi za Bunge zipo katika mpango wa kuelimisha wananchi namna shughuli za Bunge zinavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na kuwaeleza wajibu wa mbunge kwa mwananchi.