Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Maisha ya wanawake 400 yaboreshwa Temeke kupitia mradi wa MWEI.

$
0
0

003.mwei temeke

Meneja wa Vodacom Foundation kupitia mradi wa MWEI, Grace Lyon, akiwahakiki baadhi ya kinamama wajasiriamali wadogowadogo wanaofanya biashara katika soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI wakati walipokuwawakikabidhiwa fedha zao za mikopo hiyo.

001.MWEI-TEMEKE

Meneja Mawasiliano wa  Vodacom Tanzania,Bi.Rukia Mtingwa(katikati)akiongea na baadhi ya kinamama wajasiriamali wadogowadogo wanaofanya biashara katika soko la Temeke Sterio jijini Dar es  Salaam wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI.

004.mwei temeke

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa kulia akishuhudia Asha Omari kushoto wa Kikundi cha Umoja ni Nguvu akihesabu fedha kiasi cha shilingi Lakimoja baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi,Nikufya Mbengomwanja( katikati) wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI.wakati walipokuwawakikabidhiwa fedha zao za mikopo hiyo.

005.mwei temeke

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa( kulia) akishuhudia Karunde Mussa wa Kikundi cha uuzaji wa Mbogamboga katika Soko la Temeke Sterio jijini Dar es Salaam, akihesabu fedha kiasi cha shilingi Lakimoja baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi,Nikufya Mbengomwanja( katikati) wakati walipofika sokoni hapo kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa kinamama hao kupitia mradi wa MWEI wakati walipokuwa wakikabidhiwa fedha zao za mikopo hiyo.

* MWEI yafikia wilaya 42 Tanzania Bara na Visiwani

* Shilingi milioni 327/- zimetolewa hadi sasa

Wanawake 400 wanaofanya biashara ndogo ndogo  katika wilaya ya Temeke , jijini Dar es Salaam,  wamenufaika  na mikopo yenye thamani ya shilingi milioni thelathini  itakayowawezesha kuendeleza biashara zao wilayani humo.

Mikopo  hiyo isiyokuwa na riba imetolewa na mfuko wa jamii wa Vodacom (Vodacom Foundation) kupitia mradi wake wa kuwawezesha wanawake kiuchumi (MWEI.)

Akizungumza  katika shughuli  ya kukabidhi mikopo hiyo iliyofanyika katika eneo la Temeke Stereo, Meneja Mradi wa MWEI Grace Lyon alisema utoaji wa mikopo  hiyo ni utekelezaji wa azma ya  kampuni ya Vodacom  ya kuwawezesha  wanawake kiuchumi ili waendelee kuwa nguzo muhimu katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Lyon alisema,  “Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa Mwei imekuwa ikielekeza Nguvu zake vijijini ambako tayari tumewafikia wanawake wengi katika mikoa mbalimbali, sasa tumeona ni vema mafanikio yale yawafikie na wanawake wa mijini ambao nao kimsingi wanahitaji kujengewa uwezo wa kumudu maisha.”

Hadi sasa tumeweza kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 327katika wilaya arobaini na mbili za Tazania Bara na Visiwani.

Aidha, amesema mafanikio makubwa ambyao wanawake wa vijijini wameyapata kupitia MWEI ni matokeo ya kujituma kwao, kuamini katika kidogo kufikia kikubwa na uaminifu katika urejeshaji w a mikopo hiyo jambo ambalo limesaidia kuwafikia wanawake wengi zaidi ndani ya muda mfupi.

Mradi huo wa Mwei  hutumia teknolojia ya M-pesa  ambayo  huwawezesha  wakopaji kufanya marajesho kwa njia ya huduma hiyo jambo ambalo linamrahisishia mkopaji kupokea na  kurejesha mkopo.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara hao wa Temeke wameelezea kufurahishwa  kwao na mpango hao hasa katika kipengele cha kutokuwepo kwa riba katika mikopo hiyo.

Kwa kweli tumekuwa na changamoto ya kupata mikopo lakini hata fursa za ukopeshaji zilizopo zinatukwaza na uwepo wa viwango vya juu vya riba, hapa tunapata kwa gharama nafuu na tunarudisha mkopo bila riba, tunashukuru kwa hilo, “alisema Mfanyabiashara wa Duka katika Soko hilo Tausi Mjape

Naye Nuru Njovu ambaye ni mfanyabiashara wa vitunguu katika soko hilo  kwa upande wake ameshauri Vodacom kuwafikia wanawake wengi zaidi kwani itawakomboa wanawake katika lindi la umasikini.

 

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles