Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

PSPF kupitia PSS yazidi kuchimba hadi mizizi katika kufanikisha kuwafikia wananchi kwa urahisi

$
0
0

unnamed

Afisa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji.H.Jamadary akizungumza namna yakuweza kufaidika na uchangiaji wa hiari katika mfuko wa pensheni wa PSS.

Leo katika kuendelea kuchimba kwa mizizi kwa  kuwapa elimu wananchi mbalimbali mfuko wa pensheni wa PSPF katika mpango wa kuchangia kwa hiari Pss umeweza kuwafikia wananchi wa Tandika na mashirika mbalimbali wameweza kuhudhuria katika semina hiyo iliyo andaliwa na mfuko huo

Semina hiyo ililenga katika wafanya biashara wa aina mbalimbali ambao hujulikana kama wajasiliamali ambapo kufuatiwa kwa wafanyabiashara hao kufika na kuweza kupata elimu nayo kampuni ya Tandika Grain Agents Plc ambayo inajishughulika na uuzaji wa nafaka mbalimbali iliweza kufika na wanachama wake ili kupata elimu itakayowasaidia katika kuendeleza biashara yao na maendeleo ya familia zao.

Akizungumza na wanachama walio hudhuria semina hiyo Afisa mufuko wa Pensheni wa PSPF Bw.Hadji Jamadary ambaye ndiye aliye kuwa akitoa maelezo katika semina hiyo alianza kwa kuwafahamisha mfuko wa pensheni wa PSPF ni nini na kuweza kuwapa utangulizi wa wa semina hiyo ambayo ilikuwa ikilenga uchangiaji wa hiari (PSS).

Vilevile aliweza kutoa ufafanuzi wa namna ya kujiunga ,manufaa utakayo yapata endapo utajiunga na mfuko huu wa PSPF kwa mpango wa hiari PSS ambapo aliwaeleza kuna namna ya mafao ambayo unaweza ukachagua ili kuweza kuendelea kuchangia ambapo aliyataja mafao  hayo ambayo ni Fao la elimu, fao la ujasiriamali,fao la uzeeni,fao la kifo,fao la ugonjwa na fao la kujitoa aliweza kutoa ufafanuzi katika kila fao ambapo kwakuwa semina ilikuwa na wafanyabiashara aliweza kuwa fundisha kuhusu fao la ujasiliamali na faida zake .

unnamed (2)

Mmoja wa wanachama akifuatilia kwa makini maelezo ya majibu baada ya kuuliza swali ambalo lilijibiwa na maofisa wa mfuko wa pensheni kuhusu uchangiaji wa hiari Bw.Rashidi Iloko.

Baada ya kutoa maelekezo hayo wafayabiashara waliruhusiwa kuuliza maswali na kuweza kuchagua na kujiunga na mpango huo wa hiari .

Nao wafanya biashara hususani katika kampuni ya Tandika Grain Agents Plc Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw.Hassani Matibula aliweza kuwashukuru waelimishaji na waandaaji wa semina hiyo hususani  mfuko wa PSPF kuweza kuwafikia sehemu waliko na kuwafungu kwakuwa hawakuweza kupata watu watakao kuja na kuwapa elimu ya kuwajenga katika biashara zao alitoa wito kwa wafanya biashara wenzake waweze kujiunga ili waweze kupata manufaa na kuhifadhi sehemu salama kwa fedha zao.

Mpango huu umeanzishwa na PSPF kwaajili ya kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi.

unnamed (3)

Bw.Hemed Abdullah akiwa makini kufuatilia.

unnamed (4)

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tandika Grain Agents plc Bw.Hassani Abdallah Matimbula.

unnamed (5)

Afisa masoko PSPF Debora Danniel akiwagawia vipeperushi vikiwa vina elezea PSS mfuko wa hiari.

unnamed (6)

Afisa masoko Akiwa katika usajili wa wanachama walio weza kujiunga na mfuko wa hiari.

unnamed (7)

unnamed (8)

unnamed (9)

Zoezi la upigaji picha likiwa linaendelea kwa walio jaza fomu za kujiunga na mfuko wa huari PSS.

unnamed (10)

unnamed (11)

Baadhi  ya wanahisa wa chama cha Tandika Grain Agents Company plc.

unnamed (12)

Maofisa wa mfuko wa penshe wakitoa shukrani kwa wanachama walio weza kuhudhuria semina,kutoka kushoto ni Debora Danniel na kulia ni Hadji Jamadary.

unnamed (13)

Picha ya pamoja baadhi ya wanahisa na maofisa wa mfuko wa pension PSPF.

unnamed (1)

Debora Danniel afisa masoko PSPF ambaye alikuwa akifanya zoezi la kusajili wanahisa wa kikundi cha Tandika Grain Agents Company PLC baada ya semina.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles