Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo yaliyofanyika Kibara, mkoani Mara. Pia semina hiyo ilishirikisha viongozi wa vijiji, vyama pamoja na madiwani lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa sheria na kanuni za uchimbaji wa madini. Aliyekaa katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mhe. Kangi Lugora. Kushoto ni Kamishna Msaidizi – Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo Mhandisi Fredy Mahobe.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Mhe. Stephen Masele akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Mtalaamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akiwasilisha mada wakati wa semina hiyo.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Sekretarieti ya maandalizi ya semina hiyo ikiwajibika.