Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Muungano wetu unahitaji meza ya majadiliano na maridhiano

$
0
0

Maoni ya Mhariri

Tahariri

MOblog Tanzania

JUZI Waziri Kivuli wa Muungano na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Mbunge Tundu Lissu aliitaka serikali kutoa maelezo bungeni, kuhusu sababu za kuuawa kwa waasisi wa sita wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanaodaiwa kuzikwa katika handaki moja Zanzibar.

Lissu alikuwa akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Msemaji huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani aliitaka serikali kueleza waasisi hao walifanya makosa gani.

muungano 1

Nyerere na Karume wakibadilishana nyaraka muhimu za muungano.

Kwa maoni yetu hayo yaliyopita si Ndwele mbali tugage yajayo kwa sababu kuturudisha nyuma kwa sasa si hoja kwani haina mashiko bali ni kwa sasa kati ya watanzania bara na visiwani kuweka msimamo wa pamoja ili kuamua mustakabali wao juu ya muungano wanaoutaka.

Lakini kwa upande mwingine sisi katika MOblog tunamuunga mkono Mbunge Lissu kwa kusema sasa si wakati wa kuendelea kudaganyana ni wakati muafaka kwa viongozi wa sasa na wa zamani kuwaelezea watanzania nini dhumuni la muungano, matatizo yapo wapi? Hati ya muungano ipo wapi? Ili watanzania wajue aina ya muungano ambao wanao na wanataka muungano wa aina ngani? Isitoshe muungano ni wa wananchi si wa viongozi.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki alitumia nafasi hiyo kunukuu nyimbo ya mwanamuziki maarufu wa reggae, Hayati Bob Marley wa ‘Get up Stand up, stand up for your right’ ambapo kwenye nyimbo hiyo gwiji hilo la muziki wa reggae alisema kwamba ‘you can fool all the people sometime but you cannot fool all the people all the time’ kwa tasfiri ya kawaida ni kwamba unaweza kuwadanganya watu wote kwa kipindi Fulani lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote.

Lissu alisema kwamba wao kizazi cha Muungano wanataka kujua ukweli wa mambo kuhusu muungano lakini alihoji uhalali wa nchi kubwa Tanganyika kuitawala nchi dogo Zanzibar kimabavu nasi tunasema umefika wakati wa viongozi wetu kuwa na meza ya maridhiano kati ya pande mbili hizi yaani bara na visiwani.

Kwani bila maridhiano ya dhati kabisa hakuna muungano bali kila siku kukicha kutakuwa na malalamiko kutoka pande zote mbili nafasi tunayo hasa kwenye mchakato wa kuandika katiba ni sehemu muafaka wa kusahihisha makosa waliofanya waasisi wa muungano ili tuwe na muungano wenye tija na uliorithiwa na watanzania wote bara na visiwani,

Lissu pia aliibua mambo mazito kuhusu mgawanyo wa fedha za misaada na mikopo ya kibajeti kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Muungano pics 7

Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume wakitiliana saini.

Alikwenda mbali na kuitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar au Wazanzibari kwa umoja wao, kufungua kesi Mahakama za kimataifa kudai fedha zote ambazo nchi yao imeibiwa kwa kivuli cha Muungano.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alisema hadi Machi mwaka huu, Zanzibar ilikuwa imepata gawio la Sh27.1 bilioni badala ya Sh32.6 bilioni zilizoidhinishwa na Bunge, sawa na asilimia 83.

Hata hivyo, alisema hilo linaweza lisiwe tatizo, kwani kwa mwelekeo wa takwimu hizo, hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wa fedha, gawio lililoidhinishwa linaweza kuwa limelipwa lote.

Haya hivyo, alisema tatizo kubwa na la msingi ni kwamba, gawio lililoidhinishwa na Bunge si halali kwa Zanzibar, kwa mujibu wa hotuba ya Waziri wa Fedha, Saada Mkuya ya Aprili 30, mwaka huu

Hayo yote ni mambo mazito yanayohitaji busara, hekima, unyenyekevu na usikivu wa hali ya juu na hata wataalamu wa kuandika katiba na wenye weledi wa hali ya juu wanahitajika katika kuyashughulikia kwa kiwango cha kuridhisha na njia sahihi ni meza ya majadiliano na maridhiano ya kitaifa kati ya nchi hizi mbili.

Asanteni naomba kuwasilisha.

Damas Makangale

Mhariri Mkuu MOblog Tanzania


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles