Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

“Pampu za solar; ufunguo wa tatizo la ukosefu wa maji”

$
0
0

pix 1

Mkurugenzi mtendaji wa Davis & Shirtliff Bw. Benjamin Munyao akimuelezea Mr. Nehemia Mchechu Director General wa NHC jinsi pampu ya maji aina ya Lorenzo inavofanya kazi. Pampu hii ya Lorenzo inayoendeshwa kwa kutumia mionzi ya jua ni nzuri kwa watanzania wengi kutokana na urahisi wa gharama za uendeshaji maana haitumii mafuta wala umeme, urahisi wa matengenezo na mengine mengi.

pix 3

pix2

Mkurugenzi mtendaji wa Davis & Shirtliff Bw. Benjamin Munyao akimkabidhi zawadi Mr. Nehemia Mchechu Director General wa NHC alipotembelea banda la Davis & Shirtliff katika maonyesho yaliyofanyika hapa jijini Dar es salaam.

Wasambazaji wa vifaa vya umeme na maji katika kanda la Africa mashariki Davis & Shirtliff Group wamewaomba Watanzania kuchagua sululisho la tatizo sugu la ukosefu wa maji na umeme. 

Haya yalisemwa na  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Davis & Shirtliff Bw. Benjamin Munyao mnamo tarehe 8 May 2014 wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonyesho ya 17 ya  Build Expo 2014.

Kama ilivyo kwa nchi nyingine maskini duniani, watanzania wamekua wakikabiliwa na tatizo la umeme na maji. Katika suala la maji; Tanzania ikiwa nchi ambayo robo tatu ya nchi na ni kame ni ngumu sana kwa watu kupata fursa ya kufikia maji masafi kama hawaishi karibu na bahari au maziwa matatu makuu zinazoko mpakani mwa nchi.

Ingawa Tanzania ina taasisi, sera na kanuni nzuri za kusimamia masuala ya maji, bado inakabiliwa na hali ya dhiki inayohusiana kwa njia moja au nyingine na ukosefu wa maji katika nyanda mbalimbali na suala hili mwishowe linaathiri uchumi na uzalishaji wa mtu.

Watanzania wamehimizwa kuzifikiria zaidi vyanzo mbadala kama umeme wa mionzi ya jua na umeme utokanao na nguvu ya upepo kupunguza uhaba wa maji na umeme, kwa maana masuala haya  mawili yana athari kubwa katika shughuli zao za kiuchumi.  

Davis & Shirtliff wasamabazaji wakubwa wa vifaa vya umeme na maji wamejikita katika sekta sita za bidhaa zao ikiwemo bidhaa za pampu za visima vya maji.  Davis & Shirtliff kupitia bidhaa zao mbalimbali kama Dayliff, Sundaya, Opti, Grundfos na Shurflo ni suluhisho la ukosefu wa maji na umeme.

Lorentz – pampu ya maji inayoendeshwa kwa kutumia mionzi ya jua ni moja ya bidhaa inayosambazwa na kampuni ya Davis & Shirtliff. Pampu aina ya Lorents ilikuwepo katika maonyesho ya 17 ya Build Expo 2014.

Sifa za kipekee kuhusu Lorentz Solar Pump ni muundo wake wa kufanya kazi ambapo ina controller ya hali ya juu yenye uwezo wa;

-Kutenga kiwango cha chini na kiwango cha juu cha kasi ya maji;

-Uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu za takwimu za uendeshaji, muda wa kuanza na kumaliza uendeshaji, kiasi cha umeme kwa muda huhifadhiwa na mashine kwa ajili ya mapitio ya baadae.

-Ina kifaa kinacholinda mashine wakati mbalimbali kwa mfano wakati umeme umezidi au umepungu, wakati joto likizidi, wakati wa kubadili mgawanyo wa maji na wakati mashine inapump sehemu ambayo maji yameisha

Kwa mujibu wa Practical Action, pampu zinazotumia mionzi ya jua ni bora kwa jamii za kijijini ambapo hali ya maisha ni ngumu na upatikanaji wa vyanzo vya umeme in finyu. Katika matumizi ya kila siku pampu zinazoendeshwa kwa kutumia mionzi ya jua, ni za manufaa kwa jamii kama hizi kutokana na

-gharama nafuu za matengenezo

-Hakuna gharama za mafuta au umeme

-Ni za ubora na uwezo wa kudumu hadi miaka 20


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles