Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Pinda kuzindua maadhimisho wa Wiki ya Elimu mjini Dodoma

$
0
0

IMG_5332

Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Elimu yatakayofanyika kitaifa mkoani Dodoma. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Magreth Kinabo.

HASSAN SILAYO- MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kesho atazindua maadhimisho wa Wiki ya Elimu Mjini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene alisema kuwa Maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na Maafisa elimu wa Mikoa kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu katika mikoa yao.

“Maadhimisho ya wiki ya elimu yatakwenda sambamba kwa taarifa mbalimbali kuhusu mafanikio katika sekta ya elimu kutolewa na maafisa elimu wa mikoa ili kuwapa fursa wananchi kujua nini kimefanyika katika sekta ya elimu”. Alisema Mwambene.

Pia Bw. Mwambene aliongeza kuwa katika maadhimisho hayo shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa zitapewa zawadi.

Aidha Mwambene aliongeza kuwa wanafunzi walioandika insha kuhusu Afrika Mashariki na SADC watapewa zawadi.

Maadhimisho hayo yatafungwa Tarehe kumi na Rais Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles