Afisa Mtendaji Mkuu wa BMTL, Copy Cat, Bw Mike Holtham akizungumza na mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe hizo za kuzindua jina jipya nchini na kuzungumza na wateja wao.
.Yapata Afisa Mtendaji Mkuu Mpya
.yawa wakala rasmi wa bidhaa za Samsung Tanzania
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
KAMPUNI ya Business Machines Tanzania Limited (BMTL) imebadilisha rasmi jina lake la biashara kwenda kwenye kampuni yake mama ya Copy Cat katika harakati zake za kupanua wigo wa biashara nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa uzinduzi rasmi wa jina la biashara la Copy Cat nchini, Afisa Mtendaji Mkuu Mpya wa Kampuni hiyo, Bw Mike Holtham amesema kampuni inayofuraha ya kujiunga rasmi katika jina la kampuni mama ya makampuni hayo ya Copy Cat Afrika Mashariki.
“kampuni ya BMTL ilikuwa ni miongoni mwa kampuni ya Copy Cat kwa hiyo viongozi wamekutana wa Afrika Mashariki wameona ni fursa ya kipekee kuunganisha au kutumia jina moja la kibiashara (Brand) katika kujiimarisha katika biashara za kompyuta na ufundi na utengenezaji wa mifumo ya mitandao na mawasiliano nchini,” amesema Bw, Holtham
Amesema kuwa kubadilisha jina la kibiashara na jambo la kawaida katika mkakati wa kujiimarisha kibishara na kimasoko katika juhudi za kutafuta wateja wapya na kupanua wigo wa biashara ili kukuza mauzo ya ndani na nje ya nchi.
Afisa Mtendaji Mkuu, Bw Mike Holtham na akiwa pamoja na Mkuu wa Mauzo, Bw Avais Ansari wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kwenye sherehe hizo zilizofanyika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar hivi karibuni.
Bw. Holtham aliongeza kuwa kwa zaidi ya miaka 2o kampuni ya BMTL ilikuwa chini ya kampuni ya Copy Cat na imewakilisha vizuri katika soko la Tanzania kwenye maswala ya teknolojia na kompyuta.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mauzo, BMTL, Copy Cat, Avais Ansari amesema kuwa kwa zaidi ya miaka 50 kampuni hiyo imejikita kwenye maswala ya ulinzi wa kutumia teknolojia na uchapaji wa vitu mbalimbali kwa kutumia kompyuta hapa nchini.
“kubadilisha jina na kwenda kwenye kampuni mama ya Copy Cat ni mkakati tu kwa kibiashara katika jitihada ya kukuza na kupanua biashara zetu hapa Tanzania,” amesema Bw, Ansari
Amesema kampuni hiyo ipo pia katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia na Tanzania na wana mkakati wa kwenda nchi zingine kusini mwa jangwa la sahara.
Mkuu wa Mauzo, Bw Avais Ansari akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Bw. Holtham akigonganisha glass na baadhi ya wateja wa kampuni hiyo hapa nchini.
Baadhi ya wateja wakibadilishana mawazo kwenye sherehe hizo mahsusi kwa wateja.