Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Rais Putin wa Russia atengana na mkewe baada ya ndoa iliyodumu kwa miaka 30.

$
0
0

a_560x375

Rais Vladimir Putin wa Russia ametengana mkewe Lyudmila Alexandrovna baada ya kuishi maisha ya ndoa kwa miaka takriban 30.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 30 na mkewe wametoa tangazo hilo katika televisheni ya taifa.

Mkewe Lyudmila mwenye umri wa miaka 55 ambaye alimuoa mwaka 1983 alikuwepo pembeni yake wakati rais akitangaza kutengana kwao.

Akijibu maswali alipoulizwa iwapo kwa sasa wanaishi tofauti rais huyo alisema ‘ndio’ na kuongeza kuwa kazi zake zinahusiana na kuonekana kwa jamii kila mara huku watu wengine wanapenda na wengine hawapendi.

Amesema muda mrefu wamekuwa hawaonani na kila mtu amekuwa akiishi maisha yake kutokana na ratiba ya kazi zake.

Rais huyo na mkewe wana mabinti wawili Maria na Yekaterina ambao wote wanamiaka zaidi ya 20.

Lydmila amewahi kuonekana mara chache sana katika kipindi chote ambacho mumewe amekuwa katika nafasi za juu za kisiasa nchini humo.

Mara ya mwisho kuonekana pamoja hadharani ni wakati wa sherehe za kumuapisha Putting kuiongoza nchi hiyo kwa awamu ya tatu Mei 7 mwaka jana.

Wanandoa hao walioana Julai 28 mwaka 1983 wakati Putin akiwa afisa kijana katika shirika la kijasusi la KGB na mkewe akiwa mfanyakazi wa ndani ya ndege.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles