Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Maadhimisho ya Kimataifa ya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kufanyika tarehe 7 Aprili

$
0
0

01

 Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Dkt. Ben Rugangazi akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya maadhimisho ya Kimataifa ya kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994, maadhimisho hayo yatakayofanyika jijini Dar es salaam Aprili 7, mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Ofisi ya Rais (Asiye na Wizara Maalum), Prof.Mark Mwandosya.

02

 Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Dkt. Ben Rugangazi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es salaam kuhusu kumbukumbu ya maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994. Kushoto ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo.

03

Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Dkt. Ben Rugangazi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya  kumbukumbu ya miaka 20 ya  mauaji ya kimbari ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994, maadhimisho hayo yatakayofanyika jijini Dar es salaam Aprili 7, mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi kwa maandamano kuanzia New World Cinema karibu na kituo cha mabasi ITV kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Ofisi ya Rais (Asiye na Wizara Maalum), Prof.Mark Mwandosya. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene.

05

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene wakati wa mkutano na MBalozi wa Rwanda nchini Tanzania Dkt. Ben Rugangazi jijini Dar es salaam.

04

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Dkt. Ben Rugangazi (kulia) mara baada ya kikao na waandishi wa habari jijini Dar es salaam. Katikati ni Katibu wa Ubalozi wa Rwanda nchini Ernest Bugingo.(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Latest Images

Trending Articles



Latest Images