Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Smile communications Tanzania, Lawrence Ndimbo akimpigia simu mmoja wa washindi wa promosheni ya Shinda iPad katika droo ya mwisho iliyoendeshwakatika makao makuu ya Smile Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa masoko wa Smile Linda Chiza na katikati ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdalla Hemed.
Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Smile Communications Tanzania, Lawrence Ndimbo akimkabidhi zawadi ya Min iPad Richard Sawere ambaye aliibuka mmoja wa washindi wa promosheni ya shinda iPad iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo mwezi Machi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Masoko wa Smile Linda Chiza. Jumla ya iPad 13 zimetolewa katika shindano hilo.
Kampuni ya Smile communications Tanzania (Smile), inayoongoza kwa kutoa huduma za internent Dar es Salaam na Arusha, leo imeendesha droo ya mwisho katika droo za wiki kuhitimisha promosheni yao ya “Shinda iPad” ambapo wateja 13 wenye bahati wamejinyakulia iPad kila mmoja.
Katika ofa hiyo, wateja wapya wa Smile walitakiwa kununua kifaa cha Mi-Fi au Router kutoka katika maduka au vibanda vya Smile ndani ya mwezi Machi ili kupata nafasi ya kushindania moja kati ya iPad 13 zilizokuwa zikishindaniwa.
Promosheni hiyo iliyokuwa ikisimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (TGB) imewazawadia wateja tisa (9) kutoka Dar es salaam na (4) kutoka Arusha. Droo ya mwisho imefanika leo makao makuu ya Smile Dar es Salaam ambapo washindi wanne wa mwisho wamechaguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Linda Chiza, amesema kampuni yake imetoa zawadi ya toleo jipya la iPad lililowezeshwa katika tekinlojia ya 4GLTE zikiwa na vivurushi vya GB5 za intaneti.
“ Tunawapongeza washindi na wote walioshiriki na kutembelea kwenye sehemu tunazotolea huduma” alise Chiza na kuongeza kuwa “ kila mwezi tunakuwa na kitu cha kuwafanya watabasamu tutawajulisha nini kinafuata.