Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Alexander Ng’winamila akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaa, Shule ya Biashara (UDBS) hawapo pichani wakati wa semina kuhusu kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza, iliyoandaliwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Bw. Moremi Marwa na katikati ni Mkuu wa Idara ya Fedha Dkt. Esther Ishengoma.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Alexander Ng’winamila , Mkuu wa Idara ya Fedha Dkt. Esther Ishengoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Bw. Moremi Marwa wakati wa semina kuhusu kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza, iliyoandaliwa na Soko la Hisa na Mitaji la Dar es Salaam (DSE) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakifuatilia maada kutoka kwa wataalam wa DES hawapo pichani wakati wa semina kuhusu kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza, iliyoandaliwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) jijini Dar es Salaam. DSE imeanzisha shindano ambalo linatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza na kupata uelewa mkubwa kuhusu masuala ya soko la hisa na mitaji.(Picha na Frank Shija, MAELEZO).