Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kesho anatarajiwa kuifungua rasmi barabara ya Mkata – Handeni ambayo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami. Barabara hii ina urefu wa kilometa 53.2.
Akiwa Wilayani Handeni, Rais Kikwete ataifungua pia barabara ya Korogwe – Handeni ambayo vile vile imekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hii ina urefu wa kilometa 65.
Katika hatua nyingine mnamo tarehe 24 Machi 2014 siku ya Jumatatu, Mhe. Rais ataweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara kati ya Korogwe na Mkumbara yenye urefu wa kilometa 76.
Barabara ya Mkata.
Barabara ya Msangazi.
Barabara ya Sindeni.