Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania, Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhusiana na masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini. Pamoja nae ni Ofisa Mwandamizi Habari, elimu na mawasiliano, Veneranda Malima.
Frank Mvungi-Maelezo
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imeanzisha utaratibu mpya wa kurejesha mikopo kwa njia ya mtandao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wabodi hiyo Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Mwaisobwa amesema kuanzia mwezi Septemba, 2013 Bodi hiyo ilianzisha utaratibu mpya wa kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya M-Pesa.
Mwaisobwa alisema katika kuimarisha mfumo wa urejeshaji mikopo kuanzia mwezi april, 2014 walionufaika na mikopo hiyo wataweza kurejesha kupitia Aitel Money.
Kabla ya kuanza kutumia huduma ya M-pesa, mnufaika wa mkopo anapaswa kuwasiliana na HELSB ili kupata mambo muhimu ambayo ni Taarifa ya Mkopo, (Loan statement) Kiwango cha marejesho, (Loan instalments) na Namba ya kumbukumbu (Loan number).
HELSB pia hutoa msaada kwa waombaji wa mikopo wanaopata matatizo madogo madogo wakati wa kujaza fomu kwa kutumia dawati maalum la msaada kwa wateja ambapo msaada hutolewa kwa njia ya simu siku za Jumatatu hadi Jjumaa kuanzia saambili asubuhi hadi saa 2 usiku.
Mwaisobwa alibainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili HELSB ni imani potofu iliyoenea kwamba mikopo hiyo ni ruzuku na ushirikiano hafifu na baadhi ya waajiri katika urejeshaji mikopo.
Mwaisobwa alitoa wito kwa wale wote walionufaika na mikopo kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wahitaji wengine kukopeshwa.
Tangu kuasisiwa kwake, Bodi hiyo imefanikiwa kutoa mikopo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla bodi kuanzishwa, ambapo wanafunzi wameongezeka kutoka wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi wanafunzi 97,348 mwaka 2012/2013,ongezeko hili ni sawa na wastani wa 10.4% kwa mwaka.
Mwaka
|
Idadi
ya Wanafunzi Waliokopeshwa |
Ongezeko
(%)
|
Kiasi
kilichoko-peshwa (Tshs
Bilioni) |
Ongezeko
(%)
|
2004/05 (Na
Wizara) |
16,345
|
-
|
9.9
|
-
|
2005/2006
|
42,729
|
161.4
|
56.1
|
467
|
2006/2007
|
47,554
|
11.3
|
76.1
|
35.7
|
2007/2008
|
55,687
|
17.1
|
110.8
|
45.6
|
2008/2009
|
58,798
|
5.6
|
139.0
|
25.5
|
2009/2010
|
72,035
|
18.4
|
237.8
|
28.7
|
2010/2011
|
92,791
|
28.8
|
230.0
|
24.5
|
2011/2012
|
94,533
|
2.0
|
311
|
35.0
|
2012/2013
|
97,348
|
2.9
|
335.2
|
7.2
|