Hon. Peter Kallaghe with Tanzania UK Diaspora Task Force at formation meeting.
Kufuatia hatua ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kuunda kamati ya muda (Tanzania UK Diaspora Task Force) itakayosimamia maandalizi ya Mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014, tunapenda kuwasilisha majina ya wajumbe wa kamati hiyo kwa Watanzania waishio Uingereza.
Kamati hiyo itakuwa chini ya Uenyekiti wa Bi Mariam Kilumanga akisaidiwa na Bw. Cleopa John katika nafasi ya Katibu. Aidha Bi Maxine Brown atashughulikia mawasiliano kati ya kamati na watanzania waishio nchini Uingereza.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni wafuatao:
Salim Amar: Makamu Mwenyekiti
Mariam Mungula: Makamu Katibu
Hassan Mussa: Mratibu wa Wajumbe wa Kamati
Mchungaji Mathew Jutta: Mjumbe
Kassim Kalinga: Mjumbe
Amos Msanjila: Mjumbe
Allen Kuzilwa: Mjumbe
Sheikh Rashid Saleh: Mjumbe
Watanzania waishio Uingereza mnaombwa kuunga mkono uongozi wa kamati hii katika kufanikisha mkutano wa Diaspora mwaka huu 2014. Kwa kuanzia Watanzania mnaweza kutuma maoni kuhusu mnayotarajia kuyaona kwenye Mkutano wa Diaspora mwaka 2014 kwa kujaza fomu ya utafiti iliyopo kwenye anuani ifuatayo : https://www.surveymonkey.com/s/5VVGK9Z
Aidha mawasiliano na Kamati yanaweza kufanyika kupitia mitandao ya kijamii ifuatayo:
Facebook: www.facebook.com/tanzaniauk
Twitter: @tanzaniaukdiasp
Barua Pepe: TanzaniaUKDiaspora@gmail.com
L-R: Chairwoman Mariam Kilumanga with Director of Communications Maxine Brown.
Men of the Task Force L-R: Allen Kuzilwah, Sheikh Rashid A. Saleh, Salim Amar, Apostle Mathew A. Jutta, Kassim Kalinga.
Taskforce in action.
Full Taskforce L-R: Hassan Mussa, Sheikh Rashid A. Saleh, Allen Kuzilwa, Maxine Brown, Mariam Kilumanga, Mariam Mungula, Kassim Kallinga, Salim Amar, Apostle Mathew A. Jutta.