Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mawaziri wasitokane na wabunge

$
0
0

PG4A2542

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba akiwasilisha Rasimu ya Katiba  mpya mbele ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, bungeni mjini Dodoma Machi 18, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PG4A2567

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya  Mabmadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) baada ya Mwenyekiti huyo kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya bele ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bungeni Mjini Dodoma Machi 18, 2014.Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge  Maalum la Katiba, Samia Suluhu (kuli), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Profesa  Anna Tibaijuka,  Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (watatu kushoto) na  watatu kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani  , Mathias Chikawe. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Na  Zamaradi Kawawa, Maelezo Dodoma

Mwenyekiti aw Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba ameliambia bunge Maalum la Katiba linaloendelea mkoani Dodoma kuwa Rasimu ya Katiba mpya inapendekeza Mawaziri wasitokane na wabunge.

Amesema hatua hii inamuondoa Rais kwenye bunge kwani kwa kuwa na Mawaziri ndani ya bunge Hilo kunalifanya bunge kushindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa kuwa serikali ni sehemu ya bunge Hilo.

Amesema Mawaziri watateuliwa na na Rais na kuthibitishwa na bunge . Aidha , rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Rais achaguliwe kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote .

Rais Mara baada ya uchaguzi na kutangazwa na Tume ya uchaguzi anaweza kufikishwa mahakama ya rufaa kuhoji uhalali wake na mgombea yeyote wa kiti hicho aliyeshindwa na Shauri hilo kuamuliwa ndani ya mwezi mmoja.

Jaji Warioba amesema Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwepo na ukomo wa wabunge wa miaka 15 ya kukalia kiti hicho mfululizo ili kuondoa dhana ya umiliki wa ubunge na kuimarisha uwajibikaji.

Hakutakuwepo na uchaguzi mdogo endapo Mbunge atafariki badala yake nafasi hiyo itazibwa na jina litakalokuwa kwenye orodha zilizoandaliwa na vyama vya siasa vyenye wabunge husika na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.

Aidha, Spika na Naibu Spika hawatatokana na Mawaziri, Naibu Waziri na wabunge ili kupata viongozi ambao hawataelemea upande wowote.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles