Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Kituo cha uwekezaji chafanikiwa kusajili Miradi 9,442

$
0
0

1

Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Pendo Gondwe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhamasishaji wa Uhamaishaji wa kituo hicho John Mnali na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO, Frank Mvungi.(Picha na Hussein Makame-MAELEZO).

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili miradi 9,442 tangu kuanzishwa kwake hadi 2013.

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa TIC, Pendo Gondwe wakati wa mkutano na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam.

Gondwe alisema kuwa  Watanzania wamekuwa na muamko katika uwekezaji ambapo katika miradi yote miradi ya Watanzania ni asilimia 52  na 25 ni miradi inayomilikiwa kwa ubia kati ya wageni na watanzania.

Aliongeza kuwa asilimia 23 ni miradi iliyowekezwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali ambapo alisema miradi ambayo inaongoza kwa  uwekezaji  ni Kilimo, Maliasili, Miundombinu, Nishati, viwanda na biashara, Usafirishaji, Elimu, Afya, Miundo mbinu na madini.

2

Meneja Uhamasishaji wa Uhamaishaji wa kituo hicho John Mnali akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Pendo Gondwe.

Alisema TIC inawahamasisha Watanzania kujitokeza kuwekeza katika miradi mbalimbali ili kusaidia katika kukuza uchumi wa Taifa.

Gondwe alisema TIC imekuwa na utaratibu wa kuhamasisha wananchi kushiriki katika uwekezaji katika sekta nmbalimbali ambapo kituo hicho kimekuwa kikitumia mikutano na makongamano kuhamasisha wananchi kusajili miradi yao.

Kituo cha  uwekezaji kinatoa huduma mbalimbali kwa ajili ya wawekezaji wa ndani kupitia dirisha moja yaani ONE STOP CENTRE  ikiwemo kuandikisha kampuni, kujisajili na VAT, TIN, na leseni mbalimbali.

3

Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Pendo Gondwe, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani, kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhamasishaji wa Uhamaishaji wa kituo hicho John Mnali.

4

Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Pendo Gondwe, akizungumza na kituo cha Televisheni One baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.

5

Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la The Citizen, Henry Mwangonde akiuliza jambo wakati wa mkutano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Hussein Makame-MAELEZO).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles