Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Balozi Seif Idd awafariji wananchi waliokumbwa na maafa ya mvua maeneo ya Wilaya ya Mjini

$
0
0

234

Moja ya kati ya Nyumba  tatu zilizoathirika na upepo mkali uliovuma na kuathiri nyumba mbali mbali katika Mtaa wa Kwaalamsha Mjini Zanzibar.

Jamii Nchini imetahadharishwa kuwa makini katika kipindi hichi kilichoanza cha msimu wa mvua za masika ambacho kimezoeleka kuwa na matukio mbali mbali ya maafa yanayoleta athari kwa wananachi.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwafariji wananchi waliokumbwa na maafa kufuatia Upepo Mkali ulioambatana na mvua jana  jioni katika maeneo ya Kwaalamsha, Makadara na Mkele ndani ya Wilaya ya Mjini.

236

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole baadhi ya Wananchi ambao nyumba zao zilikumbwa na upepo mkali katika Shehia za Kwaalamsha, Makadara na Mkele Wilaya ya Mjini.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mbali ya mvua na upepo lakini kipindi hichi cha masika pia hukumbwa na miripuko ya maradhi tofauti ya kuambukiza jambo ambalo jamii inapaswa kujihadhari nayo.

Aliwahakikishia wananchi hao kwamba Serikali Kuu kupitia Idara yake ya Maafa ambayo iko chini ya Ofisi yake inaendelea kufanya tathmini na hasara iliyowakumbwa wananchi hao na baadaye iangalie namna ya kusaidia nguvu zitakazowawezesha  kurejea katika  mazingira yao ya awali.

245

Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar akiangalia jengo la Duka la Mfanyabiashara Khadija Ame Abdulla katika Mtaa wa Kwaalamsha ambalo limeangukiwa na nguzo ya umeme kufuatia Upepo mKali uliovuma katika eneo hilo.

“ Nimekuja na Timu yangu Katibu Mkuu, Mkurugenzi Maafa na timu yake kuanza tathmini na maafa haya na baadaye kuandika ripoti itakayotusaidia sisi Serikalini namna ya kuchukuwa hatua za kukabiliana na maafa hayo yaliyojitokeza “. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi mbali mbali waliojitolea nguvu, maarifa na hata hifadhi  ya dharura kwa wenzao  waliopatwa na maafa hayo kufuatia upepo huo wa ghafla.

Alisema kitendo hicho mbali ya kuleta faraja kwa waathirika hao pamoja na Serikali kwa jumla lakini pia kimeongeza upendo na kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Wananchi hao.

“ Ukweli nimefarajika sana kusikia kwamba majirani zenu walikuwa pamoja na nyinyi muda wote wa tukio hili. Huu hasa ndio ujirani mwema unaotakiwa kuwemo ndani ya nyoyo za wanaadamu wakati wote “. Alifafanua Balozi Seif.

249

Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma  na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).

Wakitoa shukrani zao kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baadhi ya wananchi hao walioathirika na upepo huo walielezea kufarajika kwao na hatua zilizochukuliwa na majirani zao katika kuwasaidia kukabiliana na maafa hayo.

Nyumba zipatazo Tatu katika Shehia ya Kwaalamsha, Tano Sheria ya Mkele na nyengine kadhaa ambazo bado idadi yake hajijajuilikana katika Shehia ya Makadara zimeathirika kutokana na upepo huo.

251

255

257


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Latest Images

Trending Articles


MUSIC STATION – 2017.09.01


Waves Complete v2019.02.14 Incl Emulator-R2R


Practice Sheet of Right form of verbs for HSC Students


CalCen


MCGEE, SAMUEL O., DECEASED, OF...


WordPress: Reverse Shell


Adikavi Nannaya University AKNU Degree/UG Results 2017


Alison Moyet - Alf (Deluxe Edition) (2016) flac


Dynamic SQL Analytic Privilege in SAP HANA


6 Must Visit Children’s Clothing Markets in China



Latest Images