Mtaalam wa Mitandao ya Kijamii George Katoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutoa tuzo kwa wateja wake bora walioshiriki zaidi katika kurasa za Facebook na Twiiter za kampuni hiyo mapema leo. Kushoto ni Meneja wa Ubora wa Huduma kwa Wateja Tigo Mwangaza Matotola na Mtaalam wa Mitandao ya Kijamii kutoka Tigo Bi. Samira Baamar.
Mtaalam wa Mitandao ya Kijamii kutoka Tigo Bi. Samira Baamar (wapili kulia) akimkabidhi zawadi ya simu ya kisasa na cheti ya shukuruni kwa mshiriki bora wa Facebook na Twitter katika kurasa za Tigo Faudh Kiobya mapema leo jijini Dar es Salaam. Katikati yao ni Meneja wa Ubora wa Huduma kwa Wateja Tigo Mwangaza Matotola na Mtaalam wa Mitandao ya Kijamii Tigo Bw. George Katoto (kulia).
Mshindi wa pili wa mshiriki bora wa Facebook na Twitter katika kurasa za Tigo Davidy Daud Luoga akikabidhiwa zawadi na Meneja wa Ubora wa Huduma kwa Wateja Tigo Bi. Mwangaza Matotola mapema leo.
Washindi katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo.
Tigo Tanzania leo imetoa tuzo za simu za kisasa kwa wateja wake kumi bora walioshiriki katika utoaji maoni, ushauri kwa kampuni hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii ya Facebook na Twitter mwaka 2013.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao jijini Dar es Salaam, Mtaalam wa Mitandao ya Kijamii Tigo, George Katoto, amesema tuzo hizi ni kwa ajili ya kuwatambua na kuwashukuru wateja hao kumi kwa ushiriki wao katika utoaji maoni kwa kampuni, marafiki na jamaa zao kupitia mitandao ya Facebook na Twitter ya kampuni ya Tigo mwaka uliopita.
“Kwa sasa tuna wafuasi zaidi ya 332,000 katika Facebook na zaidi ya wafuatiliaji14,700 katika Twitter. Idadi hii ni nzuri na iliyotupa msukumo wa kutoa shukrani zetu kwa wafuasi wetu na wafuatiliaji wa mitandao yetu ya kijamii. Michango yao imekuwa chachu katika kutuletea ufanisi mkubwa mwaka wa 2013,” alisema.
Kutokana na maelezo ya Katoto, washindi saba bora walioweza kuzawadiwa simu aina ya Huawei – Y300 pamoja na modem yenye kifurushi cha mwezi mzima ni Faudhu Abbas Kiobya, Davidy Daud Luoga, Robiascos Jemedali, Mohamed Lukuvi, Hamimu Halfan, Ibrahim Juma na Ally Ibrahim.
Watatu wengine walioshinda ni Pascal Chacha, Daudi Daud na Badman Msolidi ambao nao waliweza kuzawadiwa modem yenye kifurushi cha mwezi mzima. Washindi wote pia walitunukiwa vyeti vya shukurani kutoka kampuni ya simu ya Tigo.
“Kurasa za Facebook na Twitter za Tigo zimekuwa ni jukwaa ambazo zimefanikiwa kuwavutia maelfu ya wateja kwenye mitandao kutokana na kuwa na vitu vyenye ubunifu na kufurahisha. Nafurahia sana kushiriki na marafiki na wenzangu wengine kupitia ukurasa zao. Napenda kuwashukuru sana kwa kunitambua kwa namna hii yakipekee,” alisema Kiobya, mshindi wa kwanza.
Katoto aliendelea kusema kwamba vigezo vilivyotumika katika kuwachagua washindi hao ni kuwa washiriki bora katika kuanzisha mada, kuchangia mada, kusambaza na kupiga ‘like’, pamoja na kushiriki katika ‘Live Chat’ za kurasa za Facebook na Twitter za kampuni hiyo.