Mwakilishi wa Tanzania katika mkutano huo Ndg. Phares Magesa ambaye pia ni Mkurugenzi wa ICT wa TPA akitoa mada katika mkutano huo unaondelea Brussels kwa kuratibiwa na Umoja wa Ulaya(EU).
Tanzania yashiriki mkutano wa 3 wa kamati ya kusimamia mradi wa kupashana habari ili kupambana na uhalifu baharini, 3rd Maritime Security & Safety Information Sharing for Capacity building (MARSIC ) unaofanyika kwa kuratibiwa na Umoja wa Ulaya , Brussels, Ubelgji 3-4 Machi, 2014.
Tanzania ni moja ya nchi zenye vituo hivyo vya kupashana habari (Informations Sharing Centres) kilichopo katika Mnara wa kupngoza Meli cha Feri (Control Tower) kinaendeshwa na TPA kwa kushirikiana na Sumatra na idara nyingine za ulinzi na Usalama za Serikali kiutekelezaji.
Vituo vingine vya mradi huo viko Djibouti, Mombasa – Kenya na Sanaa -Yemen katika ukanda wa bahari ya Hindi.
Baadhi ya wajumbe kutoka nchi mbali mbali wakiwa mkutanoni.