Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Bw. Norio Mitsuya, mara baada ya kuwasili katika stesheni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL) kuangalia namna usafiri wa Treni ya Dar es Salaam Unavyofanya kazi jana jijini Dar.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, akimuonyesha mchoro wa njia ya treni ya Bara na ile ya inayofanya Safari zake kutoka stesheni mpaka Ubungo Maziwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya huku wakiwa ndani ya treni hiyo, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shirika la Reli Tanzania (TRL) kujionea namna ya treni ya kutoka stesheni hadi Ubungo Maziwa inavyofanya kazi. Naibu Waziri huyo ameahidi kuwa Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) wataendelea kuisadia miradi mbalimbali ya Reli.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan, Norio Mitsuya (mwenye tai ya mistari ya Manjano) akishuka katika kituo cha Ubungo Maziwa, baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia namna treni ya Dar es Salaam, maarufu kama ‘treni ya Mwakyembe’ inavyofanya kazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Charles Tizeba (wa pili kutoka kushoto), akitoa ufafanuzi wa namna treni ya Shirika la Reli Tanzania(TRL), inayofanya safari zake kutoka Stesheni mpaka Ubungo Maziwa inavyofanya kazi pamoja na Matarajio ya Serikali katika kuimarisha usafiri huo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Norio Mitsuya leo mchana baada ya Naibu Waziri wa Japan kutembelea usafiri huo na kuona namna ambavyo Serikali yake inaweza kusaidia kuimarisha Usafiri huo.(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)