Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Jionee jinsi wateja wa Vodacom walivyojirusha kila kona ya Jiji La Dar wakati wa Sikukuu ya Krismasi

$
0
0

001 COCO

Msanii wa muziki wa kizazi kipya  kutoka kundi la TMK Wanaume “Chege “akionyesha umahiri wake wa kutawala jukwaa wakati wa Tamasha la Cheka Bombastiki lililofanyika katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei kwaajili ya wateja wao wakati huu wa sikukuu ya Krismasi. 

002 COCO

Mpiga picha Mkuu wa Gazeti la Changamoto  Albart Jackson akionesha simu aina ya Huawei Y210D yenye thamani ya Tsh. 160,000 kwa waandishi wa Habari aliyojishindia kwenye  bahati nasibu iliyowahusisha waandishi wa habari,wakati wa Tamasha la Cheka Bombastiki lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na uzinduzi wa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu wa sikukuu,Kulia ni Mtaalamu wa bidhaa na Vifaa vya simu wa Vodacom Bw.Edwin Byampanju na kushoto ni Meneja Masoko na usambazaji wa Huawei Ramadhani Hamad.

003COCO

Mmoja wa wasichana waliokuwa wakipromoti simu za Huawei akipita jukwaani huku akionyesha moja ya simu za Huawei wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik  lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa Vodacom na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu wa sikukuu, katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

004 COCO

Msanii wa kundi la Tiptop Connection Madee akiwaburudisha  mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach, wakati wa kusherehekea sikukuu ya krismasi na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei ,wakati wa Tamasha la Cheka  Bombastik  lililoandaliwa mahususi kwaajili ya wateja wa kampuni hizo.

005 DAR LIVE

Msanii nguli  wa muziki wa kizazi kipya Profesa Jay akiwapagawaisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live  uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti kwaajili ya wateja wao wakati huu wa msimu wa sikukuu ya krismasi. 

006 DAR LIVE

Kiongozi wa bendi ya muziki wa kundila la  Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuph akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa Tamasha la Cheka Mbombastik lililofanyika katika ukumbi wa Dar Live mbagala jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi Tamasha hilo liliandaliwa na Vodacom Tanzania na Serengeti.

007 COCO

Umati wa watu waliofurika katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam, wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik  lililoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwaajili ya wateja wa kampuni hiyo na kuzinduliwa kwa simu za mkononi za Huawei wakati huu wa msimu huu wa sikukuu ya krismasi, katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

008 DAR LIVE Joe

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya  Joe Makini akionyesha umahiri wake kwa mashabiki wa muziki huo wakati wa Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na  Vodacom Tanzania na Serengeti Breweries  katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam mahususi kwaajili ya wateja wao wakati wa msimu huu wa sikukuu ya krismasi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles