Mahafali ya 19 ya chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) yamefanyika ijumaa ya desemba 13 mwaka huu ambapo wahitimu katika ngazi za stashahada na cheti kwenye fani ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma, na mahuasiano ya umma wamehitimu.
Tazama picha za baadhi ya matukio wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Fabian, Dotto Mandolin Kahindi, Abushehe Nondo, Benjamin Mwangoka.
Wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Rais Mstaafu wa DASJOSO Alfred Ochali akisoma risala.
Mkuu wa Chuo cha DSJ, Joachim Rupepo akitoa hotuba yake na kumkaribisha mgeni rasmi kutoa nasaha zake.
Mgeni Rasmi Bi. Jimhada malembeka akitoa nasaha kwa niaba ya Meya wa manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa.
Wahitimu wakiwa wanasikiliza kwa umakini hotuba kutoka kwa mgeni rasmi.
Wahitimu wakiwa wanatunukiwa.
Wahitimu wakiwa wanatoa mkono wa Shukurani baada ya kutunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali.
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao.
Kutoka kushoto ni Elizabeth Lazaro akiwa na Jackline Marandu ambao pia ni wahitimu.
Wageni waalikwa wakiwa wanafuatilia kwa makini kinacho endelea katika mahafali hayo.
Kwaito time.