Kutana na mtoto Mandela mwenye umri wa miaka kumi (10) tu kutoka Tanzania ambae asubuhi ya siku ya alhamisi, 12.12.2013 majira ya saa tatu na nusu alifanya ofisi ya Ubalozi wa Afrika Kusini iliyopo mtaa wa mwaya, Masaki, jijini Dar es Salaam igubikwe na hamasa kubwa kiasi cha Katibu/Msaidizi wa Balozi na baadae Balozi mwenyewe, Thanduyise Chiliza kukutana ana kwa ana na mtoto huyo mahiri na kuongea nae kwa kirefu juu sio tu jina lake likumbushalo ‘’Jabali la Afrika’’ lakini pia ustadi, kipaji, ufasaha na uelewa mkubwa alioonyesha mtoto huyo wa kitanzania kwa kumuelezea vilivyo Mzee Mandela, falsafa na jinsi yeye alivyoguswa kama Mwafrika.
Kwa hakika kwa kila aliemsikia na kumuona mtoto huyo akimuelezea na akielezea alivyoguswa na kifo cha kiongozi shujaa na alama ya kimataifa dhidi ya ubaguzi wa rangi, umaskini na udhalimu duniani, alisisimka kama si kuzizima na alitabiriwa mengi makubwa siku za usoni ikiwemo na Mheshimiwa Balozi Thanduyise Chiliza (pichani) aliemtabiria makubwa na hasa katika tasnia ya uongozi wa baadae wa bara hili jadidu la Afrika.
Pichani, picha kadhaa za mtoto Mandela alipoenda kumuaga na kutoa heshima zake za mwisho kwa Tata, Dalibhunga, Khulu, Rolihlahla, Alama ya Amani, Usamehevu na Umoja Duniani, Nelson Mandela.
Mtoto Mandela akisalimiana na Balozi wa Afrika Kusini, Mh Balozi Chiliza.
Akisaini kitabu cha kumbukumbu ya Shujaa wa Dunia.
Amandlaaaaa Aweeeeeethu.
Hakika ilikuwa ni siku ya historia, Mbunifu Nguli, Manju Msita, Mh Balozi Chiliza na mtoto Mandela pichani.
Mazungumzo ya Mh Balozi na mtoto Mandela yalipokolea.
Mh Balozi akiagana na mtoto Mandela baada ya mazungumzo ya kina.
Mtoto Mandela na Tata Madiba.