Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Wanahabari wahimizwa mahusiano mema miongoni mwao

$
0
0

E83A4520

Mwenyekiti wa maadili wa bodi ya UTPC na mwandishi wa habari wa ITV mkoani Kigoma, Deo Sokolo (wa pili kushoto),akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa dharura kati ya baadhi ya wajumbe wa bodi ya UTPC na wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida.Anayeangalia kamera,ni Mkurugenzi mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan.(Picha na Nathaniel Limu).

E83A4516

 

Na Nathaniel Limu

WANACHAMA wa Klabu ya Waandishi wa Habari (Singpress) Mkoani Singida wamehimizwa kuimarisha na kudumisha, mahusiano mazuri baina yao ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo endelevu ya klabu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa Bodi ya Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC) Tanzania, Deo Sokolo  akizungumza kwenye mkutano wa dharura kati ya kamati ya utendaji ya klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida na baadhi ya wajumbe wa bodi ya UTPC. Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Singpress mjini Singida.

 Amesema mshikamano na mahusiano mazuri baina ya wanachama wa chama au Klabu yoyote ndio dawa pekee inayoweza kustawisha klabu au chama husika.

 “Lakini pakiwepo na migogoro au migongano ya aina yo yote ikiwemo ya maslahi, Klabu au chama cho chote haikitakuwa na maendeleo katu”, amesema Sokolo na kuongeza;

 “Klabu yenu ya Singpress ipo vizuri kimaendeleo kwa hiyo msije mkaruhusu maendleo hayo yadumazwe”.

 Sokolo ambaye pia ni mwandishi wa habari wa ITV mkoani Kigoma alitumia fursa hiyo kuiasa kamati ya utendaji ya Singpress  kuhakikisha upendo na  uvumilivu unadumishwa ndani ya klabu ili klabu iendelee kusonga mbele kimaendeleo.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan aliiagiza Singpress kuwaondoa mara moja kwenye Klabu watu wanaojiita waandishi wa habari wakati hawana chombo cha habari cha kukitumikia.

 “Mtu ye yote ambaye hana chombo cha habari anachokitumia, huyo sio mwandishi wa habari na hana sifa ya kuwa mwanachama wa klabu ya waandishi wa habari. Klabu yo yote ya waandishi wa habari , jukumu lake ni kuwaondoa bila kusubiri mkutano mkuu kwenye uanachama, hadi hapo watakapopata chombo cha kukitumikia na wanakuwa waandishi wa habari ‘Active’,alifafanua Karsan.

 Aidha, amesema UTPC inasikitishwa na Singpress kwa kitendo chake cha kutokuchangamka katika kubuni na kuanzisha miradi itakayosaidia kuiendeleza klabu na wanachama wake.

 “Kamati ya utendaji mimi niwaombe tu, kwamba msitarajie mratibu wa kalabu ndiye pekee atakayebuni miradi kwa ajili ya klabu yenu.  Kila mmoja wenu awe kiongozi au mwanachama, ashiriki kubuni mradi kwa maendeleo ya klabu na wanachama”,amesema.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles