Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Maonyesho ya Tanzania Buildex International Trade Exhibition kufikia tamati leo

$
0
0

DSCN9663

CEO wa TRADEX Corporation, Frank A.P.M Bruurs, akionesha wateja (hawapo pichani) namna ya bidhaa zao zinazopatikana Netherlands na Ujerumani- s-Hertogenbosch wakati wa maonesho ya Tanzania Buildex International Trade Exhibition, Mlimani City.

Na Andrew Chale

Maonyesho ya Tanzania Buildex Internatinal Trade Exhibition January 29 -31, yanayoendelea ndani ya ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Conference, yanatarajia kufikia tamati jioni ya leo.

Maonyesho hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya  kigeni kutoka falme za kiarabu  ya S.K.M Air Conditioning LLC na wadau wengine yameshirikisha makampuni zaidi ya 50 ya ndani na nje ya Tanzania ambapo wameonyesha bidhaa zao hizo pamoja na kuuza.

Baadhi ya makampuni yaliyoshiriki kwenye maonesho hayo ni pamoja na kampuni ya huduma za Internet ya Simba Net (T) LTD, TRADEX  Corporation, Choice International wasambazaji wa bidhaa za Lontor, ISTSL Limited, Rehoboth, Fairy Delights,  Afri Vision, Dello Enterprises Ltd wasambazaji wa vifaa vya SKF, SATA Ltd, na mengine mengi.

Makampuni hayo ni yale ya bidhaa za ujenzi, vifaa vya magari, vitu vya ndani, bidhaa za viwandani, maofisini na sehemu mbalimbali pamoja na makampuni ya bidhaa tofautitofauti.

DSCN9680

Direct Sales Agent wa SimbaNET, Lilian Godfrey (kushoto) akiwa na Deusdedit Msafiri  wa SimbaNET, wakiwa kwenye maonesho ya Tanzania Buildex International Trade Exhibition, Mlimani City.

DSCN9690

irect Sales Agent wa SimbaNET, Lilian Godfrey  akionesha moja ya huduma za SimbaNET FIBER, wanazotoa, wakati wa maonesho ya Tanzania Buildex International Trade Exhibition, Mlimani City.

DSCN9706

Managing Director wa Dello Enterprises Ltd, Daniel Kirahi ambao ni wasambazaji wakuu wa bidhaa za SKF za mitambo ya mashine, magari na vifaa vya viwandani, akionyesha moja ya bidhaa hizo, kwenye maonesho ya Tanzania Buildex International Trade Exhibition, Mlimani City.
DSCN9723
Custormer Support Executive wa kampuni ya SME Ltd  wa bidhaa za SATA, Waqas Ahmed  akionesha bidhaa za kampuni hiyo kwenye  maonesho ya Tanzania Buildex International Trade Exhibition, Mlimani City.

DSCN9700

Maofisa wa  ITS Limited, kutoka India na Tanzania, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maonesho ya Tanzania Buildex Internatonal Trade Exhibition, Mlimani City.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles